VETA yajipanga kukuza ubunifu na ujuzi wa ufundi kufikia Dira ya Taifa 2050

Na Tatu Mohamed, Dodoma

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Profesa Sifuni Mchome amesema VETA itaendelea kuhakikisha Watanzania wa ngazi mbalimbali wanapata elimu na mafunzo ya ufundi ili kuwawezesha kujiajiri, kuajiriwa na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Akizungumza Agosti 7, 2025 alipowatembelea katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Profesa Mchome amesema lengo la VETA ni kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji ya soko na yanawasaidia wananchi katika maisha yao ya kila siku.

“VETA ni ya kila mtu. Leo nimetembelea banda letu kuangalia shughuli mbalimbali za maonesho haya yanayofanyika kila mwaka, lengo likiwa kuonyesha ubunifu na maendeleo tunayoyafanya. Tumeona hatua kubwa katika ubunifu, ikiwemo matumizi ya nishati ya umeme, na maonesho yajayo yatakuwa na ubunifu zaidi,” amesema Profesa Mchome.

Amesisitiza kuwa wadau wa VETA wanapaswa kwenda kwenye uzalishaji mkubwa wa bidhaa zinazobuniwa ili zitumike kwa wingi na kuchangia uchumi wa Taifa, akibainisha kuwa taasisi hiyo ni sehemu ya mchakato wa kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameweka fursa nyingi katika uchumi, lakini wanawake bado hawajazitumia ipasavyo.

“Kuna vyuo vya VETA, lakini wanawake wangapi wanachukua hatua ya kujifunza ujuzi wa ufundi? Namshukuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA kwa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi ya kujifunza ujuzi unaowakomboa kiuchumi,” amesema Senyamule.

Ametoa wito kwa wanawake kutumia fursa zilizopo, akieleza kuwa ujuzi wa ufundi ni maarifa ya haraka yanayoweza kuwasaidia kupata ajira au kujiajiri na kujipatia kipato.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

Hizi ndizo hisia dhidi ya INEC, Msajili wa Vyama vya Siasa

KATIKA safu hii wiki iliyopita niliandika uchambuzi nikihoji, ‘INEC, Msajili wa Vyama wanaweza kutupa...

More like this