Tamasha la Singeli Agosti 2 wasanii kutoa burudani ya Kimataifa

Na Winfrida Mtoi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amesema wamefanya maandalizi yakutosha ya Tamasha la Muziki wa Singeli kuhakikisha wageni waliokuja nchini kwa ajili ya michuano ya CHAN wanapata burudani ya kipekee.

Akizungumza na waandishi wa leo Julai 31, 2025, jijini Dar es Salaam akielezea maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Msingwa amesema wageni wakitoka kuangalia soka wanahamia kucheza singeli upande wa pili.

” Hii ni moja ya shughuli ambayo inafanywa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kipindi hiki cha CHAN. Tumeona tusinde kinyonge baada ya mechi ya Taifa Stars na Burkina Faso, tutashusha bonge la tamasha la singeli ili wageni waliotoka nchi mbalimbali waje waone muziki wenye asili ya Kitanzania,” amesema Msingwa.

Aidhs ameeleza kuwa katika kuendelea kuupaisha muziki huo kimataifa, Serikali imeanza kutuma maandiko kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) ili kuutambua kama urithi wa Taifa.

Msingwa amesema kwa sasa Tanzania hakuna muziki unaopendwa watu wengi, wenyeji na wagenj kama ilivyo Singeli.

“Tumegundua hakuna ‘vibes’, linalofikia muziki wa singeli katika muziki wote Tanzania. Wazungu wanachanganyikiwa ukipigwa, wanacheza na kuimba huku hawajui wanaimba nini.

” Ni muziki unaozalisha ajira kwa vijana, lazima tuupromote, tuulinde na maeneo wanayofanya vibaya tutawarekebisha ili dunia ijue kuwa asili ya singeli ni Tanzania,” amesema Msingwa.

Kwa upande wake msanii wa Singeli, Manfongo, ameeleza walivyofurahishwa na fursa hiyo na kuahidi kutoa burudani kabambe kwa wageni na watanzania watakaofika siku hiyo.

“Niwaambie tu watanzania wenzangu wajitokeze kwa wingi siku ya ufunguzi wa CHAN na sisi tumejipanga vizuri kuwapa burudani ya kutosha kwenye tamasha la Singeli,”

Wasanii zaidi ya 15, wajarajiwa kutoa burudani siku hiyo, wakiwamo Dogo Paten, Miso Misondo, Wamoto Musik, Mbosso, Shoro Mwamba na Meja Kunta.

spot_img

Latest articles

Rais Samia: Kituo cha EACLC kitaimarisha uchumi wa Taifa

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema...

Vyombo vya habari vyatakiwa kuripoti habari za Uchaguzi Mkuu kwa usahihi

Na Tatu Mohamed VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuwa makini katika kuripoti taarifa zinazohusu...

Maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum UVCCM yamekamilika

Pichani ni Viongozi wa sekretarieti ya Umoja wa Vijana CCM wakikabidhi vifaa mbalimbali wezeshi...

INEC: Hakuna atakayeachwa nyuma kwenye Uchaguzi Mkuu 2025

Na Tatu Mohamed TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema imeweka mazingira wezeshi...

More like this

Rais Samia: Kituo cha EACLC kitaimarisha uchumi wa Taifa

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema...

Vyombo vya habari vyatakiwa kuripoti habari za Uchaguzi Mkuu kwa usahihi

Na Tatu Mohamed VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuwa makini katika kuripoti taarifa zinazohusu...

Maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum UVCCM yamekamilika

Pichani ni Viongozi wa sekretarieti ya Umoja wa Vijana CCM wakikabidhi vifaa mbalimbali wezeshi...