Uchaguzi Mkuu kufanyika Oktoba 29, Wapiga Kura milioni 37 wajiandikisha

Na Mwandishi Wetu

OKTOBA 29, 2025 ndio siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa Tanzania Bara ambapo Jumla ya Wapiga Kura 37,655,559 wamejiandikisha.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa TumeHuru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele leo Julai 26, 2025 kwenye hafla ya uzinduzi wa ratiba ya uchaguzi iliyofanyika kwenye makao makuu ya Tume, Njedengwa jijini Dodoma.

“Tarehe 09 Agosti, 2025 hadi tarehe 27 Agosti, 2025 itakuwa utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais. Tarehe 14 Agosti, 2025 hadi tarehe 27 Agosti, 2025 itakuwa utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani na tarehe 27 Agosti, 2025 itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais, wagombea ubunge na wagombea udiwani,” amesema Jaji Mwambegele na kuongeza:

“Tarehe 28 Agosti, 2025 hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Bara. Tarehe 28 Agosti, 2025 hadi 27 Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za Uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema na Tarehe 29 Oktoba, 2025 siku ya Jumatano itakuwa ndiyo Siku ya Kupiga Kura”.

Akizingumza kuhusu idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo, Jaji Mwambegele amesema jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha na kuongeza kuwa idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 26.55 kutoka idadi ya wapiga kura 29,754,699 waliokuwa kwenye daftari, mwaka 2020.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Zanzibar, Wapiga Kura 725,876 wapo katika Daftari la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na wapiga kura 278,751 wameandikishwa na INEC kwa kuwa hawakuwa na sifa za kuandikishwa na ZEC.

“Katika idadi ya wapiga kura 37,655,559 waliopo katika daftari, wapiga kura 36,650,932 wapo Tanzania Bara na wapiga kura1,004,627 wapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa kati ya wapiga kura hao, 18,943,455 ni wanawake sawa na asilimia 50.31 na wapiga kura 18,712,104 ni wanaume sawa na asilimia 49.69 na wapiga kura 49,174 ni watu wenye ulemavu.

Amesema jumla ya vituo 99,911 vitatumika kupigia kura ambapo vituo 97,349 vitatumika kwa ajili ya kupigia kura kwa Tanzania Bara na vituo 2,562 vitatumika kwa ajili ya kupigia kura kwa Tanzania Zanzibar.

“Idadi hii ya vituo 99,911 ni sawa naongezeko la asilimia 22.49 ya vituo vya kupigia kura 81,567 vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020,” amesema.

Jaji Mwambegele ametoa wito kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yatakayotolewa na Tume.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...