Mwinjilisti awatoa hofu watanzania kuhusu uchaguzi mkuu, kuhubiri kesho Temeke

Na Winfrida Mtoi

Mwinjilisti wa Kanisa la EAGT, Mwanza, Diana Dionizi amewatoa hofu watanzania kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu kwa kusema tayari Mungu amemwandaa kiongozi ambaye ni faida kwa Taifa.

Ameyasema hayo leo Julai 26, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Injili utakaofanyika kesho Julai 27 hadi Agosti 3, 2025 kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke ambapo yeye ndiye mhubiri mkuu.

Mwinjilisti wa Kanisa la EAGT, Mwanza, Diana Dionizi(kulia), akiwa na Mchungaji wa Kanisa la EAGT Temeke wakati alipowasili, akipokelewa na viongozi na waumini wa kanisa hilo.

Ameeleza hakuna shaka Rais atapatikana na viongozi wote watakaotakiwa watasimamishwa kwa sababu tangu zamani imekuwa ikifanyika hivyo.

“Uchaguzi utakuwa wa amani na furaha, wasiogope. Kitu ambacho watanzania wanatakiwa wajue, sisi tunaweza tukachagua lakini Mungu ameshachagua mtu wake kabla ya sisi. Kwa hiyo Mungu atasimamisha yule ambaye ni faida kwa ajili ya watanzania na faida kwa ajili ya Taifa la Tanzania,” amesema.

Aidha amesema dunia inakwenda kwa kasi sana, hivyo kanisa linatakiwa kusimama kwa imani, pamoja na maombi.

“Siku hizi za mwisho unatakiwa kukaa kwa kutulia na kuchagua lililojema kutokana na kuwepo wingi wa Injili zinazohubiriwa ,” amesema.

Naye Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Temeke, Christomoo Ngowi amewataka watu kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo ili kupata huduma zilizoandaliwa pamoja na maombezi kwa wenye shida mbalimbali.

Kwa upande wake Mratibu wa mkutano huo, Joshua Isack amesema siku ya kesho hadi Jumapili ijayo kutakuwa kwaya na waimbaji mbalimbali mkutanoni wakiwamk John Lissu, Joel Lwaga na Boaz Dunken.

spot_img

Latest articles

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Dkt. Jafar Seif: Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba larahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za...

More like this