Meja Masai: Mashindano ya Lina PG Tour yamekuwa ya kipekee

Na Mwandishi Wetu

NAHODHA wa Klabu ya gofu ya TPDF Lugalo, Meja Japhet Masai amewapongeza waandaaji wa mashindano ya Lina PG Tour ambapo amesema kwa mara ya kwanza yamefanyika katika klabu ya Lugalo Dar es Salaam kwa weledi mkubwa.

Mashindano hayo ambayo ni kwaajili ya kumuenzi mchezaji gofu timu ya taifa ya wanawake marehemu Lina Nkya yalifanyika kuanzia Julai 17 hadi 20, 2025 na kukutanisha wachezaji zaidi ya 150, kati ya hao 68 ni wachezaji wa kulipwa na ridhaa huku 82 wakiwa wachezaji wasindikizaji.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga kwa mashindano hayo, Meja Masai amesema mashindano hayo yamefanyika vizuri na kutoa fursa kwa wachezaji kutoka sehemu mbalimbali nchini kushiriki.

Amesema pamoja na michuano hiyo kufanyika vizuri anawaomba wachezaji wa gofu kuendelea kudumisha upendo na mshikamano ili kuhakikisha mchezo huo unazidi kukua na kuimarika nchini.

“Watu wamejitokeza kwa wingi na tumejifunza mambo mengi hasa ushirikiano ulioneshwa, tumeshuhudia uimara wa uwanja wa Lugalo hivyo tunawapongeza wale wote walioshinda na kuwataka ambao hawakushinda kujipanga upya na mashindano yajayo,” amesema Meja Masai.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mashindano hayo na Mkuu wa familia ya Nkya, Said Nkya amesema kuwa mashindano hayo yalikuwa ni kwaajili ya wachezaji wa gofu wa kulipwa na ridhaa lakini wamewaingiza wachezaji wasindikizaji ili kukuza pia vipaji vyao.

Katika michuano hiyo mshindi wa kwanza kwa upande wa wachezaji wa kulipwa ni Fadhil Nkya ambaye amejipatia kiasi cha Sh. Milioni 6.8, mshindi wa nafasi ya pili ni Abdallah Yusuph aliyepata Milioni 4.3 na mshindi wa tatu Nuru Mollel aliyepata Milioni 3.4.

Kwa upande wa wachezaji wa ridhaa (Elites), mshindi wa kwanza ni Prosper Emmanuel aliyepata kiasi cha Sh. Milioni 2.2, nafasi ya pili ikichukuliwa na wachezaji wawili waofungana pointi ambao ni Julius Mwinzani na Gabriel Abel ambapo kila mmoja amepata Milioni 1.1.

Kwa upande wa wachezaji wasindikizaji mshindi wa jumla ni Ally Mwinyi, mshindi wa pili katika kundi hilo ni Maryanne Mugo, huku makundi maalum, mchezaji bora wa jumla kwa wanaume ni Abid Omari na kundi la wanawake ni Amina Nkungu.

Mshindi katika kundi la wanaume daraja A wa kwanza ni Nicholas Chitanda huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Sigfrid Urassa, katika kundi la wanaume daraja B nafasi ya kwanza ni Shukuru Sanga huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Kennedy Kajuna.

Washindi upande wa kundi Silver Division wa kwanza ni Zumla Khamis, wa pili Habiba Likuli huku mshindi wa tatu akiwa Joyce Warega, upande wa Bronze Division wa kwanza ni Anita Siwale, mshindi wa pili, Zainab Bachoo na wa tatu: Doreen Minnah.

Kundi la wachezaji wakongwe mshindi ni Gulam Dewji na kundi la watoto (Junior Category) mshindi wa kiume ni Ibrahim Hassan na mshindi wa kike ni Loyce Emilio huku katika kundi la wachezaji wapya kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mariam Rashid wa pili akiwa Sandra Kiunsi.

Katika kundi la zawadi maalum kwa wanaume mshindi aliyekaribia shimo (Nearest to the Pin) ni Femin Mabachi huku aliyepiga mpira mbali zaidi (Longest Drive) akiwa ni Brian Mbesere.Kwa upande wa wanawake aliyekaribia shimo (Nearest to the Pin) ni Zumla Khamis na aliyepiga mpira mbali zaidi (Longest Drive) ni Jazilla Daniel.

Zawadi maalum kwa mchezaji mwanamke chipukizi ikichuliwa na Hawa Wanyeche huku zawadi maalum kwa kikundi ikienda kwa kikundi cha Mkuu wa Majeshi wa zamani Jenerali mstaafu George Waitara.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...