Na Mwandishi Wetu
Mwamuzi wa Tanzania ,Ahmed Arajiga ni miongoni mwa waamuzi wa wameteuliwa kuchezesha michuano ya CHAN yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 2,2025.
Uteuzi huo wa Arajiga ni muendelezo wa kupata nafasi ya kuchezesha mashindano mkubwa, kwani amekuwa akifanya vizuri katika mashindano akisimama kama mwamuzi wa kati.
Mwamuzi mwingine kutoka Tanzania ambaye ameteuliwa kushiriki katika michuano hiyo Ally Hamdani Said, ambaye atatumika kama mwamuzi msaidizi.
Fainali za CHAN zitachezwa katika chi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, na Uganda ambapo ufunguzi utafanyika Tanzania, huku mechi ya ufunguzi ikitarajiwa kuikutanisha Taifa Stars na Burkina Faso kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.