Jessica: CCM inajali uongozi wa vijana

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama amesema Chama Cha Mapinduzi kinajali sana uwezo wa Vijana katika uongozi ndio maana kinawaamini na kuwapa nafasi za juu za kiuongozi.

Jessica Mshama aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Watangazi wa Kipindi cha Sentro cha Clouds Tv kilichofanyika Julai 8, 2025 katika studio za Clouds Tv Jijini Dar es Salaam.

Jessica ameonesha uthabiti wa CCM katika uongozi wake kwa kuitofautisha na vyama vingine kutokana na kuwaamini Vijana katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kwamba ushindi wa CCM hautokani kwa bahati mbaya kwa sababu kimejenga zaidi kwa Vijana.

Kuhusu suala la Uchaguzi, Jessica Mshama amesema kuwa Viongozi wa Juu wa Jumuiya ya UVCCM wamekuwa wakiratibu Mikutano inayohusisha Ziara zao katika Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha Vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali pamoja na kujiandaa kupiga kura ifikapo Oktoba 2025.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this