Rais Mwinyi atembelea Banda la Nishati Maonesho ya Sabasaba

📌Apatiwa elimu juu ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia

📌 Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa tasisi zake kutekeleza majukumu yake kikamilifu

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi leo 7 Julai, 2025 ametembelea banda la Wizara ya Nishati kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba jijini Dar es salaam.

Akiwa kwenye banda la Wizara ya Nishati Mhe Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Neema Mbuja, ambapo alimweleza juu ya hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa ajenda hiyo ni utekelezaji wa azimio la Rais Samia kama kinara wa nishati safi ya kupikia.

Amesema Wizara ya Nishati kupitia taasisi zilizopo chini ya Wizara zimekuwa zikitekeleza kwa vitendo ajenda hiyo kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambae ni kinara wa nishati safi ya kupikia kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Wizara ya nishati tayari imezindua mikakati miwili ya nishati safi ya kupikia na ule wa mawasiliano ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo.

spot_img

Latest articles

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...

Rais Samia kuzindua Dira ya Taifa ya 2050

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa...

More like this

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...