KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lameck Nyambara amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Segerea.
Kada huyo amekabidhiwa fomu hiyo leo Julai 01, 2025 katika Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi.

Akizungumza mara ya kukabidhiwa fomu hiyo, amesema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto za Jimbo la Segerea.
