Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo Cha Kodi na Mjumbe wa Seneti ya Mkoa wa Dar es Salaam Mwaka 2021/2022, amechukua na kurudisha fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.

Amanzi ameingia rasmi kugombea jimbo moja na Mbunge aliyemaliza Muda wake katika Jimbo Hilo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale maarufu Babu Tale.

Amanzi ambaye ndiye kijana pekee aliyechukua fomu katika jimbo hilo akiwa na maono makubwa huku akijidhatiti kuwatumika wananchi pindi atakapopata nafasi hiyo ndani ya chama.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu amesema vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo ameona ni muda muhimu kuweza kulitumikia taifa lake.

Amesema kutokana na utekelezaji wa ilani ya chama chini ya usimamizi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika majimbo mpaka nchi umepelekea kujitathimini na kuona anafaa kuweza kumsadia Rais kuisimamia na kutekeleza ilani ya chama kwa kuwatumikia wananchi.

“Kutokana na demokrasia iliyopo kwenye chama chetu imepelekea mimi kama kijana ambae nimejitathimini na kujipima lakini pia ninauzoefu wa uongozi ndani ya chama kuamua kuchukua fomu ili chama kikinipa ridhaa niweze kuwatumikia wananchi,” amesema Amanzi.

Mpaka sasa Amanzi ni kijana pekee aliyethubutu Kugombea Ubunge katika Jimbo hilo.

spot_img

Latest articles

DAWASA yafafanua sababu ya ukosefu wa maji maeneo ya Kibaha hadi Kisarawe

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)...

Tanesco yatambuliwa kama sekta wezeshi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

📍Yapokea cheti cha pongezi kwa mchango wake katika kuendeleza elimu jumuishi 📍Utambuzi watolewa katika hafla...

DAWASA yaanza kufunga Pampu zitakazoimarisha huduma ya Maji

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),...

TPDC Yahimiza Wananchi Kulinda Miundombinu ya Bomba la Gesi Asilia

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuwashirikisha wananchi...

More like this