Kaboyoka ajiunga rasmi na ACT Wazalendo

Na Tatu Mohamed

MBUNGE wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha 2020 hadi 2025, Nagy Livingstone Kaboyoka, amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo.

Hafla ya mapokezi imefanyika leo katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Kaboyoka amepokelewa na Kiongozi wa Chama hicho, Ndugu Dorothy Semu, pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo.

Kaboyoka ni mzoefu katika siasa za Tanzania na amewahi kushika nafasi mbalimbali zenye ushawishi.

Alikuwa Mbunge wa kuchaguliwa wa Jimbo la Same Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kati ya mwaka 2015 hadi 2020, ambapo alimshinda aliyekuwa Mbunge wa CCM, Anne Kilango Malecela.

Aidha, amehudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa miaka 10 mfululizo, kuanzia mwaka 2015 hadi 2025.

Ujio wa Kaboyoka ndani ya ACT Wazalendo unaelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha nguvu ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, hasa katika harakati za kujenga upinzani imara na chenye dira ya uwajibikaji wa kweli kwa wananchi.

spot_img

Latest articles

Serikali yajipanga kuimarisha utumishi wa umma, kuendeleza mageuzi ya kidigitali

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa...

Bokya amtahadharisha mapema Tyson wa Bongo

Na Winfrida Mtoi Bondia Ismail Khalid maarufu Boyka ametamba kutoa kipigo kikali kwa mpinza wake...

Mwili wa Jenista Mhagama Kuzikwa Jumanne Mbinga, Ruvuma

Na Mwandishi Wetu MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa...

Mradi wa upanuzi Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Kinyerezi I Extension umekamilika

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema kuwa mradi wa upanuzi...

More like this