Dk. Biteko ataka  Afrika kupewa uhuru wa kuzalisha nishati kwa kutumia rasilimali zilizopo

Na Mwandishi Maalum

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Dk. Doto Biteko ametoa wito kwa nchi za Afrika kupewa uhuru wa kuzalisha nishati kwa kutumia rasilimali zilizopo barani humo.

Dk. Biteko ametoa wito huo leo Juni 19, 2025 wakati akizungumza katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg linalofanyika nchini Urusi.

Amesema Afrika inahitaji programu itakayosaidia kufikia dhamira yake ya kuondoa idadi kubwa ya watu ambao hawatumii nishati safi huku akitaja baadhi ya athari za matumizi ya nishati isiyo safi ikiwemo uharibifu wa mazingira.

Ameongeza kuwa Afrika ina vyanzo vingi vya kuzalisha nishati, mfano Tanzania kuna vyanzo kama vile jua, maji na gesi asilia. Hata hivyo hakuna uhuru wa kutumia makaa ya mawe licha ya kuwepo kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwa nchi kubwa duniani zinaweza kufanya hivyo.

“ Hivyo iangaliwe namna kwa kila nchi kutumia raslimali zake ili kuzalisha nishati, mfumo uliopo unazifanya nchi zote kuwa sawa lakini ukweli ni kwamba hatuko sawa. Kwa mfano Afrika inachangia asilimia 3 hadi 4 pekee ya uchafuzi wa mazingira, lakini imepewa mzigo mkubwa zaidi.” amesema Dk. Biteko.

Amesisitiza kiwa  kila nchi itumie utaratibu wake wa kuzalisha nishati lakini kwa lengo la kupunguza uchafuzi wa mazingira..

Amezungumzia uhusiano mzuri uliopo wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi na kusema kuwa uendelee kuwa wa kuheshimiana na kukubaliano ambapo ametaja manufaa yake kuwa ni pamoja na kubadilishana ujuzi na kuisaidia Tanzania katika mitaji ya miradi nishati.

Amebainisha kuwa Tanzania ina mpango wa kutumia makaa ya mawe kwa ajili ya kuzalisha takribani megawati 120 za umeme.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Urusi, Sergey Tsivilev amesema kuwa Rais wa nchi hiyo  Vladimir Putin amekuwa na jitihada mbalimbali za kuhakikisha zinaungana na nchi zingine katika kupatia ufumbuzi changamoto za masuala ya nishati.

Naye, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya African Energy Chamber, NJ Ayuk amesema kuwa ni muhimu kwa nchi za Afrika na Urusi kuungana na kuhakikisha sauti ya Afrika inasikika na kutekeleza wanayokubaliana ili wote waweze kunufaika na uhusiano kati yao.

Aidha, ameiomba Serikali ya Urusi kuwezesha kampuni kutoka nchini humo ili ziweze kuwekeza zaidi Afrika hususan katika sekta ya nishati.

Pia, ameipongeza Tanzania katika hatua iliyopiga na mafanikio yake katika sekta ya nishati sambamba na kutoa wito kwa nchi za Afrika kujifunza zaidi kutokana na mafanikio yaliyopo nchini Urusi.

Jukwaa hilo la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg linatarajiwa kuwa na washiriki kutoka takribani nchi 140.

spot_img

Latest articles

DCEA yakamata Lita 66,048 za kemikali bashirifu

NA MWANDISHI WETU MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ((DCEA), imefanikiwa kukamata...

Chevron yaonesha nia ya kuwekeza Tanzania katika sekta ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI kubwa ya nishati kutoka Marekani, Chevron Corporation imeeleza utayari wake wa...

Jumba la maajabu laiponza Yanga,  yapigwa faini  milioni 30,  Meneja  matatani

Na Mwandishi Wetu KLABU ya Yanga imetozwa faini ya Sh 30 milioni  kwa kosa la...

Waziri Ndejembi atoa maelekezo mazito utekelezaji wa mradi Malagarasi MW 49.6 KIGOMA

📌Hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mkandarasi kwenye mradi 📌Aagiza ukaguzi maalum wa matumizi ya...

More like this

DCEA yakamata Lita 66,048 za kemikali bashirifu

NA MWANDISHI WETU MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ((DCEA), imefanikiwa kukamata...

Chevron yaonesha nia ya kuwekeza Tanzania katika sekta ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI kubwa ya nishati kutoka Marekani, Chevron Corporation imeeleza utayari wake wa...

Jumba la maajabu laiponza Yanga,  yapigwa faini  milioni 30,  Meneja  matatani

Na Mwandishi Wetu KLABU ya Yanga imetozwa faini ya Sh 30 milioni  kwa kosa la...