Wasira: Hatuahirishi Uchaguzi Mkuu ng’o

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitaahirisha uchaguzi ng’o kwa sababu kiliomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano na kimeongoza vizuri kwa kuleta maendeleo chini ya serikali iliyoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akiwasalimia wanachama, wapenzi wa Chama na wananchi waliofika ofisi za CCM Mkoa wa Ruvuma kumlaki akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Tuliomba ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa miaka mitano, tumeiongoza Tanzania, tumefanya kazi yetu vizuri halafu unatuambia tuahirishe, ahirisha wewe mambo yako sisi hatuwezi ng’o, sisi tunagombea, tumeshaweka wagombea, tumemuweka Daktari Samia Suluhu Hassan (mgombea urais kupitia CCM), tumemuweka Dk. Emmanuel Nchimbi (Mgombea Mwenza wa CCM).

“Sasa wako rafiki zangu wale wa ‘tone tone’ wao wanapita wanawaambia tusifanye uchaguzi na mimi nawauliza tukiacha kufanya uchaguzi nchi itakuwa inaongozwa na nani, maana huwezi kuwaambia watu acheni uchaguzi halafu huwapi mbadala eti tuahirishe, tuahirishe nini?,” alieleza na kuhoji.

Alisema kuwa kote ambako wamepita na hata ambako bado hawajapita, CCM iko imara na inamuunga mkono Dk. Samia Suluhu Hassan na hawamuungi kwa sababu zozote ambazo hazielezeki, bali wanamuunga kwa sababu ya maendeleo makubwa aliyoyafanya “haya mnayoyasikia ameyafanya Songea ndiyo hayo hayo ameyafanya Tanzania nzima,”.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...