Rais Samia asisitiza maadili kwa Jeshi la Polisi 

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan amewaasa wahitimu wa kozi ya maafisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi kuwa mabalozi wa maadili na kusaidia kukomesha vitendo vya kuomba na kupokea rushwa ndani ya Jeshi hilo.

Amesema hayo leo June 09,2025 Jijini Dar es Salaam wakati akishiriki sherehe ya kufunga kozi ya Maafisa na Wakaguzi wa Jeshi la Polisi.

“Muwe sehemu ya kukomesha vitendo vya kuomba na kupokea rushwa. Haya ndiyo maradhi makubwa yaliyokuwa ndani ya Jeshi letu. Sitaki kusema yameisha, yapo, yanaendelea. Nikirushiwa clip (inayoonesha vitendo vya rushwa), namrushia IGP, na anachukua hatua mara moja,” amesema.

Rais Samia ameliagiza jeshi hilo kuhakikisha linaimarisha maadili kwa videndo kwa maafisa na askari wake ili melinda heshima ya taasisi hiyo na kuzidi kujenga imani ya wananchi kwa combo via dola.

Amesema  mafanikio ya  Jeshi la Polishi katika kulinda  raia na mali zao hayawezi kupatikana endapo maadili kudorora miongoni mwa watendaji wake.

Kuhusu usalama barabarani amelitaka jeshi hilo kuimarisha mikakati ya kuthibiti ajali za barabarani, akisema licha ya kushuka  kwa jumla ya idadi ya ajali na vifo katika mwaka  mmoja uliopita, bado takwimu za vifo ni kubwa.

Aidha amelitaka kuongeza ubunifu na matumizi ya teknolojia kabila kudhibiti ajali hizo.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this