Tanzania na Japan zasaini ushirikiano wa uwekezaji biashara ya Kaboni

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan zimetia saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni nchini Tanzania.

Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 28, 2025 Tokyo, Japan kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Asao Keiichiro (Kei).

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu na hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Amesema mashirikano haya yataongeza fursa ya kupanua soko la Biashara ya Kaboni kutoka kwa wawekezaji wa Japan watakaowekeza katika miradi ya biashara ya Kaboni itakayoibuliwa nchini.

Waziri Masauni ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anawataka wataalamu kutoka nchi hizi mbili kufanya kazi haraka, kwa bidii, na kwa pamoja kwa manufaa ya nchi zote mbili ili kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yanaenda katika hatua ya utekelezaji.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa “Tuko tayari kufanya kazi kwa ukaribu na wenzetu wa Japan ili kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa faida ya nchi zote mbili.

Tayari Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeimarisha uwezo wa kitaasisi na kisheria katika usimamizi wa Biashara ya Kaboni ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais iliandaa kanuni za mwaka 2022 za kuratibu biashara ya Kaboni.

Aidha, Mhandisi Mhandisi alibainisha kuwa katika Mfumo wa Kitaasisi, Serikali imeanzisha Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira iliyofanyiwa marekebisho ya 2025.

Hafla ya utiaji saini ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja, na Watendaji kutoka Ofisi hiyo.

spot_img

Latest articles

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Na Mwandishi Pwani SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi...

SAMIA AONGOZA TAIFA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOA KWA AJILI YA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu MAMIA ya wananchi, viongozi wa Serikali na wakuu wa vyombo vya...

e-GA YASIFU MAGEUZI YA TANESCO KATIKA UTOAJI HUDUMA KIDIGITALI

📌 Wavutiwa namna TANESCO inavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kutoa huduma nzuri kwa...

KAIMU MSAJILI TPRB ASHIRIKI MAFUNZO ELEKEZI YA UONGOZI KWA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI, MASHIRIKA YA UMMA NA WAKALA ZA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB),...

More like this

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Na Mwandishi Pwani SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi...

SAMIA AONGOZA TAIFA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOA KWA AJILI YA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu MAMIA ya wananchi, viongozi wa Serikali na wakuu wa vyombo vya...

e-GA YASIFU MAGEUZI YA TANESCO KATIKA UTOAJI HUDUMA KIDIGITALI

📌 Wavutiwa namna TANESCO inavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kutoa huduma nzuri kwa...