INEC yaanzisha majimbo mapya nane

Na Mwandishi Wetu

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imeanzisha majimbo mapya nane nchini kote, ambapo jijini Dar es Salaam, majimbo mawili ya Chamazi na Kivule yameanzishwa kutokana na mgawanyo wa majimbo ya Mbagala wilayani Temeke na Ukonga Wilaya ya Ilala.

Majimbo mapya yatakuwa sehemu ya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, ambapo Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Rufani Jacob Mwambegele, amesema tume yake imefikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 12 jijini Dodoma, Jaji Mwambegele amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 75(1), (2) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 18(7) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024.

Ameyataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Kivule amabalo limegawanywa kutoka Jimbo la Ukonga na Jimbo la Uchaguzi la Chamazi lililogawanywa kutoka Jimbo la Mbagala yote ya mkoani Dar es Salaam.

“Mkoani Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Dodoma Mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba na Mkoani Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Mbeya Mjini limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Uyole,” amesema.

Jaji Mwambegele ameongeza kuwa, Mkoani Simiyu limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la uchaguzi la Bariadi Mjini.

“Huko Geita yameanzishwa majimbo mawili, Jimbo la Busanda limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Katoro na Jimbo la Chato likigawanywa pia na kuanzishwa Jimbo jipya la Chato Kusini.

“Mkoani Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Itwangi,” amesema Jaji Mwambegele.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...