G. 55 rasmi wajitoa Chadema

Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu na wanachama wengine wa chama hicho wametangaza kujitoa katika chama hicho kwa madai ya kutoridhishwa na yanayoendelea.

Wametangaza uamuzi huo leo Mei 7, 2025 jijini Dar es wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

Akitangaza uamuzi huo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, Benson Kigaila akiwa pamoja na Salumu Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita, amesema wamejitoa lakini hawaendi CCM.

Kigaila amesema muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia na sasa wanashauriana na vyamba mbalimbali.

“Sisi tumeamua wote kwa pamoja kujiondoa Chadema ili tuwaachie hicho chama waendeshe wanavyotaka. Hatuwezi kuwa wanachama wa chama ambacho maamuzi yake hayafanywi kwa vikao.

“Hatuwezi kuwa wanachama ambao wanabaguliwa.Katiba haifuatwi, sisi sio chawa, sisi tunajitambua, tuliingia Chadema malengo na tunatoka Chadema kwa sababu malengo yameisha basi tunawaachia chama chao,” ameelaza Kigaila.

Kwa upande wake Mwalimu amesema alikuwepo katika chama hicho kwa muda mrefu na hakufuata vyeo wala fedha bali aliamini kwamba kama mtoto wa Taifa hili ana kila sababu ya kutoa mchango wake nchini.

spot_img

Latest articles

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....

Dkt. Mataragio: Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wanaoficha mafuta

Na Tatu Mohamed SERIKALI imetoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo vya kuficha...

Lukuvi afariki dunia

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye...

Mgodi wa kihistoria wa niobium kujengwa Mbeya

Na Mwandishi Mbeya TANZANIA imepiga hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Marekani baada...

More like this