Majaliwa: Serikali inathamini kazi inayofanywa na sekta

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na sekta binafsi katika kuimarisha ustawi wa jamii nchini.

Amesema hayo leo Ijumaa (Mei 02, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miaka 100 na mkutano wa 100 wa Rotary International District 9214 kanda ya Tanzania na Uganda, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.

“Serikali yetu imedhamiria kuendelea kukuza ushirikiano wa dhati na wana-Rotarian wote ili kwa pamoja tuendelee kukuza ustawi wa Tanzania,” amesema.

Amesema kuwa kazi kubwa zinayofanywa na Club ya Rotari zimesaidia kuboresha hali za maisha ya wenye uhitaji kwenye sekta ya afya, maji na elimu.

Amesema juhudi zao zimeonekana kuanzia uchimbaji wa visima vijijini, uwekaji wa samani na ukarabati wa shele na kuweka vifaa katika vituo vya afya.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa hivi karibuni Mheshimiwa Dkt. Samia alitunukiwa tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” kutokana na matokeo makubwa ambayo yamepatikana kwenye uongozi wake ikiwemo kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80.

“Zaidi ya hayo, katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, Serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa ufadhili wa huduma za afya, kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, na kujenga zaidi ya vituo 530 vya kujifungulia ili kupunguza vifo vya uzazi, vifo vya watoto wachanga na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano,” amesema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Daniel Sillo amesema kuwa Wizara hiyo inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rotari nchini.

“Hata hivyo ninawakumbusha umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya usajili yaliyowekwa na msajili wa jumuiya za kijamii,” amesema.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this