Balile: Waandishi wa habari zingatieni utaratibu mnapotimiza majukumu yenu

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amewataka waandishi wa habari kote nchini kufuata utaratibu na misingi ya taaluma wanapotekeleza majukumu yao, hususan wakati wa kuripoti kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 02, 2025 jijini Dar es Salaam, Balile amesisitiza umuhimu wa kuwa na vitambulisho halali vya kazi pamoja na kuvaa jaketi za uandishi kama alama za utambuzi zitakazowasaidia kutekeleza majukumu yao bila bugudha.

“Waandishi wa habari hawapaswi kuzuiwa kufanya kazi zao za kukusanya, kuchakata na kuhabarisha umma. Niwaombe waandishi kuondoa woga na kuzingatia misingi ya taaluma kwa kutoa taarifa sahihi na zenye uhalisia,” amesema Balile.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha waandishi wanalindwa na kutambuliwa vyema na vyombo vya dola wakati wa kuripoti kesi hiyo itakayosikilizwa Mei 6, mwaka huu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Balile amebainisha kuwa baada ya vurugu zilizotokea awali mahakamani, alifanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, ambapo walikubaliana kuwa kila mwandishi atakayetaka kuripoti kesi hiyo anatakiwa kuwa na kitambulisho rasmi au Press Card.

“Ni lazima waandishi watambulike kabla ya kuingia mahakamani. Watakaokidhi vigezo hivyo wataruhusiwa kuingia bila kuzuiwa,” ameeleza.

Hata hivyo, amewataka wanahabari kufika mapema mahakamani kwa kuwa nafasi ni ndogo na chumba kikijaa hawataruhusiwa kuingia.

Amesisitiza kuwa mwandishi yeyote atakayekumbwa na changamoto asisite kuwasiliana naye moja kwa moja.

Katika hatua nyingine, Balile amekemea tabia ya baadhi ya waandishi kutumia picha kutoka mitandaoni zisizo na uhalisia, akisisitiza kuwa hali hiyo ni hatari kwa tasnia na inaweza kupotosha umma.

“Mwandishi wa habari unatakiwa kuamini picha uliyopiga mwenyewe. Picha za mitandaoni mara nyingine hutengenezwa na si halisi,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DPC), Bakari Kimwanga, amewakumbusha waandishi kuhakikisha wanazingatia usalama wao wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Jambo la usalama ni la kwanza kisha kazi. Mwanahabari ni lazima uwe na kitambulisho na kuvaa jaketi ya kazi ili utambulike kwa urahisi,” alisema Kimwanga, ambaye pia ni Mjumbe wa TEF.

Kimwanga amesisitiza kuwa jukumu la kulinda heshima ya taaluma ya habari ni la kila mwandishi na kwamba maadili, weledi na uwajibikaji ni nguzo muhimu katika kulinda haki ya wananchi kupata taarifa sahihi.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

More like this

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...