Mwanaisha Mndeme wa ACT Wazalendo ajitosa kuwania ubunge Kigamboni

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Idara ya Mambo ya Nje wa Chama cha ACT Wazalendo, Mwanaisha Mndeme amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mndeme amesema anaingia katika kinyang’anyiro hicho kwa nia moja ya kuwatumikia wananchi wa Kigamboni kwa moyo wa dhati, uadilifu na bidii.

Amesema Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeipa mamlaka Bunge kutunga Sheria, hivyo kupitia taaluma yake ataungana na wabunge wengine kutunga Sheria zenye tija kwa wananchi wa Kigamboni na Watanzania kwa ujumla.”Bunge limepewa mamlaka ya kusimamia na kuishauri serikali.

Nitakuwa sehemu ya kuisimamia, kuishauri serikali na pia kuwa mwakilishi wa wananchi wa Kigamboni kwenye agenda zinazowahusu,” amesema Mndeme ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara wa Chama cha ACT Wazalendo.

Amefafanua kuwa, Jimbo la Kigamboni kumekuwa na changamoto za muda mrefu ikiwemo Miundombinu ya Barabara ambapo kuna Kata tatu za Kimbiji, Pembamnazi na Kisarawe 2 hazina Barabara za lami hivyo kupeleka changamoto ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo.

“Wananchi wanaoishi Kata hizi wamekuwa wakipata changamoto kufikia maeneo yao ya kupata riziki, wanafunzi kuchelewa kufika shuleni na wananchi kupata usumbufu kwenye kuifikia Hospitali ya Wilaya,” amesema na kuongeza:

“Pia Kigamboni tulikuwa na Vivuko vitatu lakini mpaka sasa kimebaki kimoja, licha ya kazi inayofanywa na Bakhresa Limited ya kuvusha wananchi kupitia Sea Tax, lakini Serikali haipaswi kukimbia wajibu wake wa kutoa huduma hii. Kwa upande wa Daraja la Mwalimu Nyerere ambalo ndilo pekee linalolipiwa, hivyo NSSF watuambie lini biashara ya kulipia inafikia mwisho,”.

Ameongeza kuwa, endapo akipata nafasi hiyo, atashirikiana kwa karibu na wananchi wa Kigamboni ili kutekeleza miradi mbalimbali ya Afya, elimu, ajira kwa vijana, miundombinu ya Barabara, usambazaji wa maji safi na salama pamoja na mazingira mazuri ya biashara na Uwekezaji.

“Ninaamini kuwa Kigamboni inahitaji kizazi kipya chenye Dira, uthubutu na maono mapana ya Maendeleo. Nimejifunza, nimejizatiti na nipo tayari kuhimili vikwazo na kuwaletea matokeo ambayo wananchi wa Kigamboni wanastahili,” amesema.

Mndeme alijiunga na Chama cha ACT Wazalendo mwaka 2018 na kufanikiwa kushuka nafasi mbalimbali ikiwemo Katibu Ngome ya wanawake Taifa (2018-2020), Katibu wa Ngome ya Vijana (2020-2024) pamoja na nafasi mbalimbali kwenye Baraza Kivuli la Mawaziri ikiwemo Waziri Kivuli wa Hifadhi ya Jamii, Waziri Kivuli wa Maji na sasa ni Waziri wa Kivuli wa Viwanda na Biashara.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...