Sh. Bilioni 30 zaidhinishwa kujenga Barabara zilizoathiriwa na mvua

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa barabara muhimu za maeneo mbalimbali nchini zilizoharibiwa na mvua.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametoa taarifa hiyo mkoani Morogoro alipokwenda kwa dharura baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kuharibu barabara inayounganisha Ifakara – Mlimba kwenda mkoa wa Njombe.

Ulega alisema pamoja na kiasi hicho cha fedha kilichoidhinishwa na Rais kwa ajili ya ujenzi wa dharura, mipango ya serikali ya ujenzi wa kudumu wa barabara na madaraja inaendelea kama ilivyo na haiathiriwi na mipango hii ya dharura.

“Nimekuja kwenu wananchi wa Morogoro – na hasa nyinyi wa Ifakara, Malinyi, Ulanga na Mlimba, kuwafikishia salamu za Rais wenu na pole zake kwa taabu hii mliyoipata. Lakini nimekuja pia na habari njema.

“Rais wenu, Samia Suluhu Hassan, amekubali matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa dharura wa barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua hizi zinazoendelea, hapa kwenu na maeneo mengine ya Tanzania, ili maisha yenu yaendelee. Barabara ni uchumi. Barabara ni maisha na lazima kazi ziendelee,” alisema.

Ulega aliyelazimika kukatisha kuendelea na vikao vya Bunge vinavyoendelea mkoani Dodoma kwa ajili ya kufanya safari hiyo ya dharura, alifuatana na baadhi ya wahandisi wabobezi nchini kutoka wizarani na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili wasimamie viwango kwenye ukarabati utakaofanyika.

Kabla ya kuzungumza na wananchi wa Ifakara na viongozi waliokuwepo kwenye eneo barabara ilikokatika, Ulega alifanya ziara kwa njia ya helikopta akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, kuona athari za mvua kwenye miundombinu ya barabara na madaraja mkoani humo.

Baadhi ya miundombinu ya Morogoro kama madaraja, itafaidika pia na mpango wa serikali wa ujenzi wa madaraja na barabara wa kudumu unaoendelea nchini baada ya miradi yake kuridhiwa na serikali ya Rais Samia.

Baadhi ya barabara za Morogoro zitakazofaidika na mpango huu wa serikali ni Ulanga – Namhanga ambayo imetengewa zaidi ya shilingi bilioni 6.3 na Malinyi mpaka Mto Fulua iliyotengewa shilingi bilioni 12.

Katika taarifa yake kwa Waziri, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima alisema mkoa wa huo ni mkubwa na maombi yao kwa serikali ni kwamba barabara muhimu zijengwe katika hali ambayo zitaweza kupitika wakati wote.

spot_img

Latest articles

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...

Rais Samia kuzindua Dira ya Taifa ya 2050

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa...

More like this

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...