Na Mwandishi Wetu
Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalifungwa na Pacome Zouzoua dk 11, Prince Dube dk 34 wakati la Azam likifungwa na Lusajo Mwaikenda dk 81.

Wakati huo huo timu ya Tabora United imepoteza mchezo wa nne mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya leo Aprili 10, 2025 kufungwa mabao 3-0 na Mashujaa FC katika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Kabla ya mchezo wa leo ilitoka kufungwa na Pamba 1-0, CCM Kirumba, Mwanza, imepoteza nyumbani dhidi ya Yanga 3-0, na JKT Tanzania iliifunga 2-1.

Nayo Coastal Union baada ya kukosa ushindi katika michezo nane mfululizo leo imezinduka kwa kuifunga Singida BS mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.