Serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu ya umeme

📌 Lengo ni kuondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme

📌 Ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Kilindi, Tanga waffikia asilimia 35.

📌Bilioni 2.63 kulipa fidia wanaopisha njia ya kusafirisha umeme Mkata- Handeni-Kilindi

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea na ukarabati wa miundombinu ya kusambaza umeme ili kuondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme nchini.

Kapinga ameyasema hayo leo Aprili 10, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Handeni Mjini, Mhe. Reuben Kwagilwa aliyeuliza ni lini Serikali itaondoa changamoto ya kukatika kwa umeme wilayani Handeni.

“Changamoto ya kukatika umeme Wilayani Handeni inatokana na uchakavu na urefu wa miundombinu ya kusambaza umeme. Katika kukabiliana na changamoto hii Serikali kupitia TANESCO inaendelea na ukarabati wa miundombinu ya umeme ikiwa ni pamoja na kubadilisha nguzo za miti na kuweka za zege,” amesema Kapinga.

Ameeleza kuwa, Serikali kupitia mradi wa gridi imara inaendelea na ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mkata, Handeni ambacho kipo kwenye hatua za awali za ujenzi.

Ameongeza kuwa, ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Kilindi, Tanga umefikia asilimia 35 na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 132 kutoka Mkata kupitia Handeni hadi Kilindi umeffikia asilimia 30.

Akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi aliyeuliza kuhusu Serikali kuona umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa vituo vya umeme vya Mkata, Lushoto na Kilindi kutokana na umuhimu wa vituo hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme Mkoa wa Tanga, Mhe. Kapinga amesema tayari Wizara ya fedha imeihakikishia Wizara ya Nishati kuwalipa wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kwa wakati ili waikamilishe.

Na kuhusu kusuasua kwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata hadi Kilindi kutokana na ulipwaji wa fidia, Mhe. Kapinga amesema fidia ya wananchi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata, handeni hadi Kilindi ni takribani shilingi bilioni 2.63 ambayo Wizara ya fedha wameihakikishia Wizara ya Nishati kuilipa fidia hiyo.

Kapinga ameongeza kuwa, fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mkata, Handeni tayari wameshalipwa fidia.

Akijibu swali la Mbunge wa Hanang’, Mhandisi Samwel Xaday aliyeuliza ni lini Serikali itatatua changamoto ya kukatika kwa umeme Wilaya ya Hanang’, Mhe. Kapinga amesema Wilaya ya Hanang’ ipo katika mradi wa ujenzi wa gridi imara awamu ya pili ambapo kitajengwa kituo cha kupokea na kupoza umeme ambapo kwa sasa Serikali inaendelea na awamu ya kwanza ya mradi wa gridi imara.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Grace Tendega kuhusu kukatika kwa umeme mkoani humo hasa Jimbo la Kalenga, Mhe. Kapinga amesema Serikali inayo mikakati ya kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Iringa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya umeme kwa kubadilisha nguzo na nyaya chakavu.

Aidha, Kapinga amesisitiza kuwa kutokea Mkoa wa Iringa, Tunduma hadi Katavi Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa kusafilisha umeme wa TAZA ambao unahusisha ujenzi wa vituo vya kupoza umeme ambavyo vitaboresha upatikanaji wa umeme maeneo yote ya ukanda huo na kuongeza kuwa mradi huo utaunganisha gridi za Taanzania na Zambia.

spot_img

Latest articles

Yanga kuikabili TRA bila Depu, kocha aeleza ugumu ulipo

Na Mwandishi Wetu WAKATI Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Machi 18, 2026  kuikabili TRA United katika Ligi...

Vijana 3,967 waomba uwezeshaji kupitia Go Green na IMBEJU ya CRDB Bank Foundation

Na Mwandishi wetu JUMLA ya vijana 3,967 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamewasilisha maombi ya...

RC Kunenge aipongeza Dawasa, awapa jukumu madiwani

Na Mwandishi wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema ushirikishwaji wananchi kwenye...

Serikali yatoa maelekezo nane kuimarisha kampuni ambazo ina umiliki hisa chache kuelekea Dira 2050

Na Mwandishi wetu, Arusha SERIKALI imetoa maelekezo nane ya kimkakati yanayolenga kuimarisha utendaji wa kampuni...

More like this

Yanga kuikabili TRA bila Depu, kocha aeleza ugumu ulipo

Na Mwandishi Wetu WAKATI Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Machi 18, 2026  kuikabili TRA United katika Ligi...

Vijana 3,967 waomba uwezeshaji kupitia Go Green na IMBEJU ya CRDB Bank Foundation

Na Mwandishi wetu JUMLA ya vijana 3,967 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamewasilisha maombi ya...

RC Kunenge aipongeza Dawasa, awapa jukumu madiwani

Na Mwandishi wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema ushirikishwaji wananchi kwenye...