DC Kibaha afungua Baraza Kuu la Wafanyakazi DAWASA

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon amefungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Akifungua kikao hicho katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Wilayani Kibaha, Nickson amewapongeza wajumbe wa baraza hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya inayopelekea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Nickson amesema uhalali wa Serikali kuendelea kuwepo ni Wananchi kupata huduma za msingi, hivyo DAWASA wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya Majisafi na Majitaka ili serikali iendelee kuwepo.

Amesema maji yanaweza kuleta amani au yanaweza kuleta machafuko, hivyo maji ni muhimu, na wanachotaka wananchi wakiomba kuunganishiwa maji, waunganishiwe kwa haraka na maji yatoke kwenye bomba.

Amesema DAWASA imeiheshimisha sana Mkoa wa Pwani kwani wawekezaji wanapokuja kutaka kuwekeza tunawaambia huduma ya maji ipo ya kutosha.

“Wawekezaji wakija Pwani sisi tunawaambia tuna uhakika wa maji na hiyo inaongeza uwekezaji katika sekta ya viwanda katika mkoa wetu, sisi kufanya vizuri Mkoa wa Pwani kunatokana na uwepo wa maji ya kutosha kutoka DAWASA,” amesema Nickson.

Mkuu huyo wa Wilaya ameitaka DAWASA kuongeza kasi na juhudi katika kutoa huduma kwa wananchi ili kufikia malengo yao na kuhakikisha wananachi wanapata huduma bora wakati wote.

“Nawaomba DAWASA muongeze speed katika kutoa huduma, kuhakikisha mnadhibiti upotevu wa maji. Wananchi wa wilaya yangu, wao wanafurahia huduma za DAWASA hivyo nawapongeza sana,” amesema.

spot_img

Latest articles

CHELSEA BINGWA WA FIFA CWC 2025

Timu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu kwa kuchapa...

Humphrey Polepole ajiuzulu

Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubalozi na...

Nandy ahamasika kutangaza Nembo ya Made in Tanzania Kimataifa

Na Tatu Mohamed MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Mfinanga (Nandy), amesema elimu aliyoipata...

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

More like this

CHELSEA BINGWA WA FIFA CWC 2025

Timu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu kwa kuchapa...

Humphrey Polepole ajiuzulu

Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubalozi na...

Nandy ahamasika kutangaza Nembo ya Made in Tanzania Kimataifa

Na Tatu Mohamed MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Mfinanga (Nandy), amesema elimu aliyoipata...