Benki ya Stanbic kuendelea kuzisaidia Kampuni ndogo za uchimbaji wa mafuta na gesi

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya Stanbic imesema kuwa itaendelea kushirikiana na makampuni madogo ya Kitanzania yanayojishughulisha na uchimbaji wa mafuta na gesi katika kuwapa uzoefu katika miradi mikubwa ijayo.

Hayo yameelezwa leo Machi 06, 2025 na Makamu wa Rais wa Miundombinu ya Nishati, Joe Mwakenjuki katika Kongamano na maonesho ya Petroli ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25) amesema wameona makampuni ya watanzania yakijitokeza katika kuangalia fursa mbalimbali katika miradi ya mafuta na gesi.

Amesema Benki ya Stanbic imeweza kusaidia makampuni hayo madogo ya kizalendo katika mnyororo wa thamani kwenye shughuli zao za mafuta na gesi.

“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia Kampuni ndogo za kitanzania katika kuwapa uzoefu katika miradi yao ya sasa wanayofanya ambayo ni midogo. Ni vema wenyewe kujipa uzoefu katika miradi ya sasa na sio kusubiri miradi mikubwa ya mafuta na gesi kufanya hata hii midogo wanaweza kufanya,” amesema Mwakenjuki.

Amefafanua kuwa Watanzania wanaendelea kujitokeza kwa wingi katika kuchangamkia fursa za miradi ya mafuta na gesi na kujiandaa na miradi mikubwa zaidi kuliko wanayotekelezwa kwa sasa.”Wanaweza kuja katika mabenki na kuweza kuwasaidia kupata uzoefu ili miradi mikubwa inapokuja tutaweza kuwasaidia zaidi kwani mahitaji ya kifedha,” amesema.

Amefafanua kuwa Stanbic Bank inashiriki kikamilifu katika kufadhili sekta ya mafuta na gesi barani Afrika kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa njia endelevu na inatoa huduma za kifedha kama mikopo, biashara ya kifedha, na ushauri kwa kampuni zinazojihusisha na mafuta na gesi.

spot_img

Latest articles

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

Jessica: CCM inajali uongozi wa vijana

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama...

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

More like this

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

Jessica: CCM inajali uongozi wa vijana

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama...

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...