JANUARI MAKAMBA AMSHUKURU RAIS SAMIA KUMFUNZA MENGI

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga Januari Makamba, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumteua  kuwa Waziri wa Nishati na Mambo ya Nje na kusema jambo hilo litaendelea kuwa historia isiyofutika katika maisha yake.

Akizungumza leo Februari 24,2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Lushoto, Tanga, Makamba amesema amejifunza mengi kupitia uongozi wa Rais Samia ameerevuka.

“Mheshimiwa Rais, naomba nikushukuru sana kutoka sakafu ya moyo wangu kwa kuniamini mimi kuniteua waziri wako, kwanza wa nishati na baadaye Mambo ya Nje ni heshima kubwa ambayo haitafutika katika uhai wa maisha yangu.

“Katika kipindi ambacho nimefanya kazi na wewe nimejifunza sana na nimeerevuka kutokana na uongozi wako. Lakini nimeerevuka sana kutokana na Uongozi wako. Lakini kabla ya hapo Mheshimiwa Rais  utakumbuka mimi nilikuwa Waziri wa Nchi chini ya Ofisi yako, tumefanya kazi wote miaka minne na ilikuwa ndiyo nafasi yangu ya kwanza kuwa Waziri, Wewe ndiyo umenifundisha kuwa Waziri, kwa hiyo kama kuna werevu nilionao basi unatokana na mikono yako na hii nitakwenda nayo kaburini kwangu,” amesema Makamba.

spot_img

Latest articles

Okello awapa jeuri mashabiki wa Yanga

Na Mwandishi Wetu Nyota wa Yanga, Allan Okello amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa watamaliza...

Minziro akabidhiwa Fountain Gate FC

Na Mwandishi Wetu KLABU ya Fountain Gate FC imemtangaza Fred Felix Minziro kuwa Kocha Mkuu...

Makonda asimamisha uongozi TOC, Rage akabidhiwa jukumu

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesimamisha uchaguzi wa...

Nani amwambie Rais Samia: ‘Name and Shame’ bila vyombo vya habari imara haifui dafu

SUALA la utawala bora halijawahi kuwa eneo rahisi katika uendeshaji na usimamizi wa ofisi...

More like this