Nchimbi awaonya wanaonza kufanya kampeni

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameonya vikali wanachama wanaotafuta uteuzi wa udiwani, uwakilishi na ubunge kwa njia zisizo halali, akisisitiza kuwa chama hakitasita kuwaengua wale watakaokiuka Katiba, Kanuni na maadili ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa makatibu wa matawi na kata kutoka Wilaya ya Dodoma, Balozi Nchimbi alisema baadhi ya wanachama wameanza kampeni kabla ya muda rasmi kwa kutumia mbinu kama kuanzisha mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kufadhili matukio ya kijamii kama kumbukumbu za misiba na sherehe za ndoa, pamoja na kushinikiza vikao vya chama kuwapitisha bila kupingwa.

“Tayari tumeshuhudia baadhi ya wabunge na madiwani wakitafuta mbinu za kuhakikisha wanapitishwa bila kupingwa. Wengine wanahamasisha matamko ya vikao, huku baadhi wakihudhuria matukio yenye lengo la kujitambulisha mapema kwa wapiga kura.

“Wapo wanaowapa posho wahudhuriaji wa mikutano wakiwa wamevaa sare za CCM ili kuonesha wanaungwa mkono. Tunawataka waache mara moja. CCM ina mfumo madhubuti wa kufuatilia mwenendo wa wanachama wake, na kumbukumbu hizi zote zinahifadhiwa. Wanaweza kushangaa majina yao yakiwekwa pembeni,” amesema.

Balozi Nchimbi amewataka madiwani na wabunge walioko madarakani kuacha kupuuza majukumu yao kwa kisingizio cha maandalizi ya uchaguzi, akisema chama kitafanya tathmini kwa kila mgombea kulingana na utendaji wake, si kwa uwezo wa kutoa fedha kwa wapiga kura.

“Tumeshuhudia watu wakichaguliwa lakini wanakaa miaka mitano bila kufanya kazi kwa sababu wanajua wapiga kura wachache wa ndani ya chama watakaowarudisha tena madarakani. Mfumo wetu mpya unalenga kumchagua mgombea kwa misingi ya kazi zake, si kwa kutumia rushwa au mbinu za kificho. Tunataka ukichaguliwa ukafanye kazi kwa wananchi,” amesisitiza.

spot_img

Latest articles

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

Serikali: Tuchukue hatua kuepuka madhara ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA)

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia kwa Mkurugenzi msaidizi, Kitengo cha Afya Moja, Ofisi ya...

Serikali yawaita wadau kujitokeza kusapoti ushiriki wa wanawake michezoni

Na Winfrida Mtoi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' amewaomba...

More like this

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

Serikali: Tuchukue hatua kuepuka madhara ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA)

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia kwa Mkurugenzi msaidizi, Kitengo cha Afya Moja, Ofisi ya...