EKARI 336 ZA BANGI ZATEKETEZWA KONDOA

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, imeteketeza ekari 336 za mashamba ya bangi yaliyokuwa ndani ya hifadhi ya Ikome Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma yakiwa yamechanganywa na mazao mengine halali ili kuficha shughuli hiyo haramu.

Akizungumza wilayani Kondoa wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo, leo Februari 18, 2025 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo ameeleza kuwa, katika operesheni hiyo, kilo 148 za mirungi zilkamatwa.

“Hii ni operesheni kubwa ya kwanza kufanyika mkoani Dodoma, ikionyesha wazi kuwa kilimo cha bangi kimeanza kuenea katika baadhi ya maeneo ya mkoa huu. Tutaendelea kuchukua hatua kali kuhakikisha kuwa uzalishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya vinadhibitiwa kwa nguvu zote,” amesema Lyimo.

Naye Fatina Ramadhani, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Haubi, amekiri kuwa baadhi ya wananchi katika eneo hilo wanajihusisha na kilimo cha bangi na amewaomba waachane na kilimo hicho, kwani matumizi ya bangi husababisha madhara mengi kwa mtumiaji.

Mkazi wa Mafai Kata ya Haubi, Abushekhe Hamis Kalinga amethibitisha kuwa, baadhi ya vijana wanajihusisha na matumizi ya bangi. “Vijana wengi walikuwa wameshaanza kuathirika, japo wengine wanadai wanalima bangi kwa ajili ya pesa lakini ukilinganisha hasara na faida, hasara ni kubwa zaidi kuliko faida. Tusipoangalia kizazi kijacho kitakuwa na watoto wasio na akili timamu,”

spot_img

Latest articles

Papa mpya apatikana ni Robert Prevost

Na Mwandishi Wetu Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69),...

Waziri Masauni, Umoja wa Ulaya wajadili Mazingira

Mwandishi Maalum-Denmark Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad...

Serikali yasamehe faini za maji, yataka wananchi warejeshewe huduma

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi...

Spika wa Bunge ateta na Dk. Mwapinga, amhakikishia ushirikiano

Na Mwandishi Wetu Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani...

More like this