Biteko aipongeza Ewura kuleta utulivu kwenye nishati

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa usimamizi thabiti wa huduma za nishati na maji nchini ambao ameeleza kuwa umechangia kuleta na kuimarisha utulivu kwenye sekta ya nishati na taifa kwa ujumla.

Biteko ametoa pongezi hizo juzi wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa EWURA kinachofanyika jijini Tanga.

“EWURA mnafanya kazi kubwa ya kudhibiti upatikanaji wa huduma za uhakika za umeme na mafuta nchini kwa ufanisi mkubwa, mmeleta utulivu kwenye sekta ya nishati nchini, mmerahisiha mazingira ya uwekezaji kwenye CNG, vituo vya mafuta vijijini na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwenye nishati safi ya kupikia, nawapongeza sana,” amesema Biteko.

Dkt Biteko amesisitiza EWURA kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kiudhibiti kuhusu ajenda ya misheni 300 ya umeme na kuwasimamia watoa huduma wanaodhibitiwa kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya huduma kwa mteja inayotekelezeka.

Aidha, aliitaka EWURA kuhakikisha inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara ya mafuta nchini, na kushirikisha wadau na watoa huduma wanaodhibitiwa kwenye maamuzi ya kiudhibiti ili utekelezaji wake uwe na tija.

Katika hatua nyingine, ametoa rai kwa EWURA kufanya tafiti za kina kuhusu huduma zinazodhibitiwa ili kubaini maeneo yanayohitaji kutiliwa mkazo, kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria ikiwamo kupokea hoja za wanaokosoa utendaji wa taasisi ili kuisaidia kujitathmini na kuboresha zaidi utendaji wake.

spot_img

Latest articles

Serikali: Tuchukue hatua kuepuka madhara ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA)

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia kwa Mkurugenzi msaidizi, Kitengo cha Afya Moja, Ofisi ya...

Serikali yawaita wadau kujitokeza kusapoti ushiriki wa wanawake michezoni

Na Winfrida Mtoi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' amewaomba...

Ndejembi awahakikishia wakazi wa Kigamboni umeme wa uhakika

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ndani ya...

Viongozi Chadema washinda shauri la kuidharau Mahakama

Na Mwandishi Wetu Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali shauri la maombi...

More like this