Muigizaji maarufu Korea Kusini, Kim Sae-ron akutwa amefariki nyumbani kwake

Na Mwandishi Wetu

TASNIA ya filamu na burudani Korea Kusini imepata pigo baada ya taarifa za kifo cha mwigizaji maarufu Kim Sae-ron (24) aliyefariki dunia nyumbani kwake jijini Seoul.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini humo, mwili wa msanii huyo uligunduliwa na rafiki yake jana Jumapili Februari 16, 2025 na kutoa taarifa Polisi.

Polisi wamesema kuwa uchunguzi wa awali haujaonyesha dalili za uhalifu, lakini wanaendelea kuchunguza mazingira ya kifo chake.

Kim alizaliwa Julai 31, 2000, na alianza safari yake ya sanaa akiwa na umri wa miaka tisa kupitia filamu A Brand New Life (2009), ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa.

Aidha aliendelea kung’ara zaidi kupitia filamu The Man from Nowhere (2010), ambayo ilimfanya kuwa miongoni mwa waigizaji chipukizi wenye mvuto mkubwa katika tasnia ya filamu ya Korea Kusini.

Katika miaka iliyofuata, alishiriki katika filamu zingine kubwa kama ‘A Girl at My Door’ (2014) na tamthilia za televisheni zikiwemo ‘Secret Healer na Leverage’.

spot_img

Latest articles

Mwigulu rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa...

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

More like this