DAWASA YAWASHIRIKISHA WAFANYABIASHARA UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewataka wafanyabiashara wanaotegemea maji katika shughuli zao, wakiwemo waosha magari, wafyatua matofali na watunza bustani, kushiriki katika kudhibiti upotevu wa maji na kulinda miundombinu ya huduma hiyo.

Wito huo umetolewa katika kikao cha kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao kuhusu matumizi sahihi ya maji, sheria na taratibu za huduma pamoja na umuhimu wa kutoa taarifa mapema kuhusu uvujaji na uharibifu wa miundombinu.

Akizungumza katika kikao hicho, Afisa Sheria DAWASA, Ezekiel Lwenge, amesema upatikanaji endelevu wa maji unahitaji matumizi yanayozingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Amewataka wateja kuepuka maunganisho yasiyo halali, kuchezea mita au kufungua na kuhamisha vifaa vya huduma bila kibali cha DAWASA.

Amesema uharibifu au kuingilia miundombinu ya maji kunaweza kusababisha usumbufu wa huduma kwa wananchi wengi wanaotegemea mtandao huo.

Kwa upande wake, Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe, Alex Ng’wandu, amesema wafanyabiashara hao wana nafasi kubwa ya kusaidia kupunguza upotevu wa maji kutokana na utegemezi wao mkubwa wa huduma hiyo katika shughuli zao za kila siku.

Amewataka kutoa taarifa kwa DAWASA wanapobaini uvujaji wa maji, uharibifu wa miundombinu, matumizi yasiyo halali au changamoto nyingine zinazoweza kuathiri huduma.

“Maji ni muhimu katika uzalishaji na shughuli za biashara. Bila maji, biashara nyingi haziwezi kuendelea, hivyo ni muhimu kila mmoja kushiriki kulinda rasilimali hii,” amesema Ng’wandu.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Bustani kutoka Mbezi Beach Africana, Jafari Mohammed, amesema elimu iliyotolewa imewasaidia kufahamu matumizi sahihi ya maji na umuhimu wa kulinda miundombinu.

Amesema wafanyabiashara wanaweza kuwa sehemu ya suluhisho la kupunguza upotevu wa maji kwa kutoa taarifa mapema wanapobaini changamoto katika miundombinu.

Naye Juma Lazaro, mfanyabiashara wa kuosha magari kutoka Kinondoni Mkwajuni, ameishukuru DAWASA kwa kuwapatia elimu kuhusu sheria na taratibu za matumizi ya huduma ya maji.

spot_img

Latest articles

TANZANIA YAZIDI KUIMARISHA NAFASI YAKE KATIKA BIASHARA YA UMEME KIKANDA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar TANZANIA imeendelea kuimarisha nafasi yake katika biashara ya umeme kikanda, huku...

MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 220 IGANJO–SAZA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA UCHIMBAJI WA MADINI – MHE. SALOME

📌 Ashuhudia utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza,...

Salome Ashuhudia utiaji saini mkataba wa sh. bilioni 198 kuimarisha umeme Songwe, Chunya

📌Ataka kasi ya utekelezaji wa mradi na wazawa kupewa kipaumbele 📌Wachimbaji wapongeza Na Mwandishi Wetu NAIBU...

ZARA TANZANIA ADVENTURES YAZINDUA RASMI KAMPENI YA TWENZETU KILELENI MSIMU WA TANO

KAMPUNI ya Zara Tanzania Adventures imezindua rasmi kampeni ya Twenzetu Kileleni – Msimu wa...

More like this