Kapinga: Kituo cha kupoza umeme cha Uhuru wilayani Urambo kimekamilika

📌 Kinalenga kuboresha hali ya upatikanaji umeme Urambo na maeneo mengine

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Uhuru kilichopo Wilaya ya Urambo mkoani Tabora umekamilika.

Kapinga ameyasema hayo leo Februari 07 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta aliyetaka kufahamu Serikali itakamilisha lini kituo hicho cha kupoza umeme na lini kitaanza kufanya kazi.

“Mhe. Spika ujenzi wa kituo cha kupoza umeme umeshakamilika, hivi sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme, ikikamilika kituo hicho kitaanza kufanya kazi,” amesema Kapinga.

Akijibu swali la Mbunge wa Nanyumbu, Ally Mhata aliyetaka kufahamu lini Serikali itashusha bei ya kuunganisha umeme katika Kata za Mangaka na Kilimanihewa kama maombi yalivyowasilishwa Wizarani, Kapinga amesema kutokana na hali halisi ilivyo nchini, kuna maeneo ya vijiji na Vijiji Miji ambapo maeneo ya vijiji yanaunganishwa na umeme kwa gharama ya shilingi 27,000.

Ameongeza kuwa, maeneo yenye sura ya Vijiji-Miji yanaunganishwa kwa gharama ya shilingi 320,960 hivyo kwa maeneo ya Kata ya Mangaka na Kilimahewa yenye sura ya Vijiji Miji yana unganishwa umeme kwa gharama ya shilingi 320,960.

Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuangalia kama kuna uwezekano wa kufanya maboresho ya gharama kutokana na tathmini iliyofanyika.

Kuhusu Vitongoji 105 ambavyo havijapata umeme Wilaya ya Nanyumbu, Kapinga amesema hivi sasa Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji ikiwemo Vitongoji 15 kwa Mbunge na kwa mwaka ujao wa fedha vitaongezwa Vitongoji vingine 38 ili kupunguza idadi ya vitongoji hivyo 105.

spot_img

Latest articles

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Na Mwandishi Pwani SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi...

SAMIA AONGOZA TAIFA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOA KWA AJILI YA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu MAMIA ya wananchi, viongozi wa Serikali na wakuu wa vyombo vya...

e-GA YASIFU MAGEUZI YA TANESCO KATIKA UTOAJI HUDUMA KIDIGITALI

📌 Wavutiwa namna TANESCO inavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kutoa huduma nzuri kwa...

KAIMU MSAJILI TPRB ASHIRIKI MAFUNZO ELEKEZI YA UONGOZI KWA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI, MASHIRIKA YA UMMA NA WAKALA ZA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB),...

More like this