TANZANIA YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIANO NA BURUNDI SEKTA YA NISHATI

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

SERIKALI imeahidi kuendelea kushirikiana na nchi ya Burundi katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya nishati.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko katika mazungumzo yake na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahim Uwizeye aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

“Rais Samia ni kinara katika kujenga mahusiano na ndani ya nchi na kimataifa, kama ilivyo kwa uhusiano kati yetu na Burundi ambayo imewezesha kutekeleza miradi kadhaa ukiwemo mradi wa umeme wa RUSUMO unaoendeshwa kwa ubia wa nchi Tatu za Rwanda, Burundi na Tanzania” amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano na Burundi na kuwataka kuimarisha mahusiano kwa wafanyabiashara ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Uwizeye amemshukuru Rais Samia kwa utayari wa kuisaidia nchi hiyo katika nyanja mbalimbali ikiwemo nishati.

Aidha, Dkt. Biteko pia amekutana na Waziri wa Nishati wa Malawi na ujumbe wake, Waziri wa Nishati wa Tunisia, Waziri wa Nishati wa Rwanda, Waziri wa Nishati wa Comoro na Rais wa kampuni ya GE VERNIVA ambao kwa nyakati tofauti wamezungumzia maaendeleo na ushirikiano katika sekta ya nishati.

Mazungumzo hayo yamekuja ikiwa ni siku moja baada ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojulikana kama misheni 300 unaolenga kuwawezesha waafrika milioni 300 barani Afrika kunufaika na nishati ya umeme ifikapo mwaka 2030.

spot_img

Latest articles

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

Jessica: CCM inajali uongozi wa vijana

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama...

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

More like this

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

Jessica: CCM inajali uongozi wa vijana

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama...

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...