Dabi ya Kariakoo Wanawake, kitaumana kesho

Na Winfrida Mtoi

Mechi ya Dabi ya Kariakoo ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara, Yanga Princess dhidi ya Simba Queens inatarajiwa kupigwa kesho saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Simba Queens inaongoza ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda michezo yake yote mitatu ilicheza hadi sasa  wakati Yanga Princess ipo nafasi ya tano na alama tatu, ikiwa bado haijaonja ushindi tangu ligi imeanza ikitoka sare mechi zote tatu ilizocheza.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake mashabiki wa timu hizo kutokana na tambo zao hasa baada ya  klabu hizo mbili kwa sasa kuamua  kutumia uwanja huo kwa mechi zake nyumbani kwa timu zote za  wanawake na wanaume.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Yanga Princess ambayo ni mwenyeji wa mchezo, Edna Lema amesema wanaiheshimu Simba kutokana na ubora wake ikiwa inaongoza ligi hiyo na haijafungwa mchezo wowote.

“Sisi hatujapata matokeo mazuri ya mechi zetu za mwanzo lakini mechi ya Dabi ina mipango yake ya kuhakikisha unapata matokeo mazuri, sisi kama timu tupo tayari kwa mechi ya kesho,”  amesema Edna.

Kwa upande wake Kocha wa Simba Queens,Yussif Basigi amesema itakuwa ni mechi ya kuvutia na mipango yao ni kuonyesha mchezo mzuri na kupata matokeo ya ushindi.

“Wachezaji wote wako fiti na tayari kwa mchezo huo.Utakuwa ni mchezo mzuri na mgumu,tunahitaji kuwa makini kwenye maeneo yote ili kupata ushindi na kujiweka mazingira mazuri ya kuendelea kuongoza ligi,” amesema  Basigi.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika uwanja huo Oktoba 02,2024 katika mchezo wa nusu fainali wa Ngao ya Jamii ambapo Yanga ilishinda kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

spot_img

Latest articles

EL NIÑO YABADILI RATIBA YA MITIHANI 2026

Na Mwandishi Wet Tishio la mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El...

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Na Mwandishi Wetu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa...

MKOA WA RUKWA MBIONI KUUNGANISHWA KWENYE GRIDI YA UMEME YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, Iringa Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya...

Akwilapo: Teknolojia mpya muhimu kukabiliana na mahitaji ya ujenzi

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo, ametoa wito...

More like this