Jay Melody kutoana jasho na Diamond, Alikiba

Na Winfrida Mtoi

Kamati ya Tuzo  za Muziki Tanzania (TMA) leo Agosti 29,2024 imetangaza wanaowania tuzo za muziki  nchini, wakianza  na vipengele vitatu ambavyo ni ni Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, wimbo bora wa taarabu wa mwaka na wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi.

Katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa mwaka, wanaowania ni Marioo kupitia wimbo ‘Shisha’, Diamond Platnumz ‘Shuu’, Harmonize ‘Single Again’, Alikiba ‘Sumu’ na Jay Melody wimbo wa ‘Nitasema’.

Vipengele vingine vilivyotangazwa  ni wimbo bora wa taarabu wa mwaka ambapo kuna  wimbo wa ‘Watu na Viatu’ wa  Malkia Layla Rashid, ‘Hatuachani’ ya Amina Kidevu, ‘Bila Yeye Sijiwezi’ ya Mwinyi ‘Mkuu, Sina Wema’ ya Mwasiti Mbwana na ‘DSM Sweetheart’ ya Salha.

Wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi kuna ‘People’ ya Libianca, ‘American Love’ ya Qing Madi, ‘Lonely at the Top’ ya Asake, ‘Unavailable’ ya Davido ft Musa Keys na ‘Mnike’ ya Tyler ICU.

Kamati ya Tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha wamesema vipengele vingine vitaendelea kutangazwa, huku mashabiki wakitakiwa kujindaa kuwapigia kura wasanii wao wanaowapenda kuanzia Septemba 3,2024.

spot_img

Latest articles

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu  SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini...

More like this

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...