Na Mwandishi Wetu, Media Brains
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugonga daraja na kutumbukia mtoni katika eneo la Mlima Myovizi, mkoani Songwe.
Ajali hiyo, iliyotokea leo Julai 15 saa 12 asubuhi, ilihusisha basi la Ngasere High Class lililokuwa likisafiri kutoka Dodoma kwenda Tunduma, mkoani Songwe.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Gallus Hyera, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo viwili na majeruhi 16 katika ajali hiyo, ambayo ilitokea baada ya basi hilo kugonga nguzo ya daraja na kutumbukia mtoni.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi, Dk. Kelvin Masae, amethibitisha kupokea majeruhi 16 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu, huku wengine wakipewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.