Waziri Kairuki aipongeza Tawa usimamizi rasilimali za wanyamapori

Na Joyce Ndunguru, Morogoro

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa usimamizi mzuri wa rasilimali za wanyamapori.

Kairuki ametoa pongezi hizo leo Julai 8,2024 wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo mkoani Morogoro kwa lengo la kusikiliza changamoto na kutoa utatuzi ili kuboresha utendaji kazi wa mamlaka hiyo.

“Nawapongeza TAWA kwa usimamizi mzuri wa rasilimali za wanyamapori kwa kuzingatia kuwa ni taasisi ambayo haina muda mrefu tangu kuanzishwa kwake,” amesema Kairuki.

Katika ziara hiyo Kairuki alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa TAWA na kusisitiza kuhusu uzingatiaji wa sheria, kanuni, miongozo na taratibu katika kutimiza majukumu yao ili kuboresha utendaji kazi.

Kuhusu changamoto ya wanyama wakali na waharibifu iliyowasilishwa na Menejimenti, Kairuki alielekeza miradi ya ujirani mwema ijikite katika kutatua changamoto hiyo kama vile ujengaji wa vizimba pamoja na utoaji wa vitendea kazi kama pikipiki ili kuzipunguza.

Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mabula Nyanda, alimshukuru, Waziri Kairuki kwa kuitembelea mamlaka hiyo na kuahidi utekelezaji wa maelekezo yote aliyoyatoa.

Awali Kaimu Naibu Kamishna anayeshughulikia huduma za uhifadhi, Mlage Kabange, alitoa taarifa kuhusu maeneo yanayosimamiwa na TAWA huku akibainisha mafanikio na jitihada zinazofanywa katika kupambana na wanyamapori wakali na waharibifu.

Katika ziara hiyo, Waziri Kairuki aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Fortunata Msoffe, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii, Abdallah Mvungi pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Wizara ya Maliasili na Utalii, Lucy Saleko.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...