Uamuzi wa serikali kuwapa wafanyabiashara vibali vya uagizaji kulishusha bei ya sukari

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa vibali vya uagizaji wa sukari kwa kampuni nyingine za wafanyabiashara kulichangia kushusha bei ya sukari kwa kiasi kikubwa hali iliyoleta ahueni kubwa kwa wananchi.

Hayo yamesemwa Julai 5,2024 na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo mchana jijini Dar es Salaam.

“Ingawa kampuni hizi za wafanyabiashara zinadhihakiwa kuwa ni za vocha, hizi ndio kampuni zilizoingiza sukari nchini kwa haraka katika kipindi kigumu cha upungufu mkubwa na kuifanya bei ya sukari ishuke,” alisema Profesa Bengesi.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Sukari Tanzania inaonyesha Kampuni za wafanya biashara zillifanikisha kuingizwa kwa sukari nyingi nchini ndani ya muda mfupi ikilinganishwa na kampuni za wazalishaji.

Ongezeko hilo lilifanikisha kushusha bei sukari nchini kutoka wastani wa Sh 7,000 mwezi Februari hadi Sh 2,800 mwezi Juni.

Bodi ya Sukari iliamua kutolea ufafanuzi hoja za upotoshaji zilizotolewa na wadau wa sukari nchini Tanzania, kwa nia ya kuondoa hofu kwa wananchi na Watanzania kwa ujumla.

spot_img

Latest articles

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...

More like this