Uhuru atoa wito kwa viongozi kuwasikiliza wananchi

Nairobi, Kenya

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametoa wito wa amani kufuatia maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 ambayo siku ya Jumanne yalikumbwa na matukio ya vurugu baada ya waandamanaji kuvamia Bunge la Taifa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Uhuru alielezea masikitiko yake kuhusu Wakenya waliouawa wakati wa maandamano, akisisitiza umuhimu wa viongozi waliochaguliwa kuwasikiliza waliowapigia kura.

“Wakati huu wa majaribu, nataka kuwakumbusha viongozi wote kwamba walichaguliwa na wananchi. Kuwasikiliza wananchi si chaguo bali ni wajibu uliowekwa katika misingi ya katiba yetu na katika misingi ya demokrasia,” alisema.

Uhuru, aliongeza kuwa serikali haifai kutumia nguvu na kuwa na upinzani dhidi ya Wakenya wanaotekeleza haki zao za kikatiba kwa maandamano ya amani.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this