VAR kutumika ligi kuu bara msimu ujao

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Ili kupunguza makosa ya waamuzi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara Serikali imependekeza kutumika kwa Teknolojia ya Kuwasaidia Waamuzi (VAR) kuanzia msimu ujao huku ikitoa msamaha wa kodi kwenye uingizaji wa mashine hizo.

Mapendekezo hayo yametangazwa Juni 13,2024 Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema VAR itasaidia kuleta ufanisi na kuhakikisha matokeo yanayopatikana uwanjani yanakuwa ya haki.

“Kuna timu msimu mmoja penati 10 halafu zikifungwa zenyewe magoli yanakataliwa, na ili tuwe na VAR za kutosha naleta penndekezo la kutoa msamaha kwenye uingizaji wa mashine za VAR na vifaa vyake,” amesema Dk. Nchemba.

spot_img

Latest articles

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...

Bidhaa ‘feki’ zadidimiza Watanzania lindi la umasikini

Watanzania wanazidi kunasa katika mzunguko wa umasikini unaosababishwa na kushamiri kwa bidhaa duni na...

More like this