Kikokotoo mafao ya Wastaafu sasa asilimia 40

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Serikali imetangaza ongezeko la malipo ya mkupuo kwa wastaafu kutoka asilimia 33 hadi asilimia 40 kwa kundi la watumishi waliokuwa wameshushwa kutoka asilimia 50 hapo awali.

Kwa muda mrefu, wafanyakazi walikuwa wakilalamikia kikokotoo cha pensheni za wastaafu kinachotumika kutokidhi hali halisi ya wanachama, wakitaka kurejeshwa kwa kanuni za zamani zilizotumika kabla ya mwaka 2017.

Msimamo huu mpya umetangazwa, Juni 13, 2024, na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema wastaafu waliokuwa wakipokea asilimia 25 hadi 33 sasa watapandishwa hadi asilimia 35. Pia, walioathirika na mabadiliko ya awali watakuwa sehemu ya mabadiliko haya.

“Serikali imesikia kilio cha watumishi na kufanyia kazi suala la masilahi ya wastaafu, Rais Samia ameelekeza kuongezeka kwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 hadi asilimia 40 kwa kundi la watumishi walioshushwa kutoka asilimia 50 hapo awali.

“Serikali itaendelea kuliangalia kwa karibu suala la masilahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko yetu,” amesema Dk. Mwigulu.

spot_img

Latest articles

YAPO MATAMANIO YA UCHAGUZI WA 2019 KUJIRUDIA 2024?

KUNA uhusiano wowote kati ya mafanikio ya kiuchumi kwa nchi yoyote na kukua kwa...

Dabi ya Kariakoo Wanawake, kitaumana kesho

Na Winfrida Mtoi Mechi ya Dabi ya Kariakoo ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara,...

Baraza la Mawaziri sasa Kidigital- Majaliwa

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki...

SOMO KUTOKA KWA WATSWANA, WAFUATA NYAYO ZA WAZAMBIA KUING’ARISHA SADC

KUNA habari njema tena kutoka ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)....

More like this