INEC YAWANOA WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGUZI JIMBO LA KWAHANI

Sehemu ya wasimamizi na wasimamizi wa Uchaguzi wasaidizi ngazi ya vituo wa Jimbo la Kwahani wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kiapo cha kutunza siri mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa mafunzo yao ya siku mbili yaliyoanza leo Juni 5 hadi 6, 2024 mkoa wa Mjini Magharibi- Unguja Zanzibar. (Picha na INEC).

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya Kupiga Kura Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar wametakiwa kufanya kazi kwa kujiamini, uadilifu na weledi wanapotekeleza majukumu yao ya uchaguzi kutokana na dhamana waliyopewa na Tume.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dk. Zakia Mohamed Abubakar wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo yanayofanyika kuanzia leo Juni 5 hadi 6, 2024 Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi- Zanzibar.

“Mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu ya Imani  ya Tume kuwa mnao uwezo wa kufanya kazi hii, Jambo muhimu mnalotakiwa kulizingatia ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, na kwamba katika utendaji wa majukumu yenu mnapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume,”amesema Dk. Zakia.

Dk. Zakia amesema, kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume imepewa jukumu la kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hii ni pamoja na Chaguzi ndogo zinazojitokeza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vifo kama ilivyotokea katika Jimbo la Kwahani.

“Hata hivyo, pamoja na kuwa Tume ndiyo yenye jukumu hilo, wanaoratibu na kusimamia Uchaguzi ngazi ya Vituo ni nyinyi tuliowateua pamoja na watendaji wengine,” amesema.

Aidha, Dk. Zakia amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndio msingi wa Uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kupunguza kama siyo kuondosha kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa Uchaguzi.

Amewataka washiriki hao wa mafunzo kuwa watulivu na kupokea mada zitakazowasilishwa, wabadilishane uzoefu na kujadili namna ya kufanikisha Uchaguzi katika Jimbo la Kwahani.

“Nachukua fursa hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katikauendeshaji wa Uchaguzi, mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea,”amesema Dk. Zakia.

Aidha, amewataka kuhakiki vifaa watakavyovipokea kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi na kuhakikisha kila Msimamizi wa Kituo anapata vifaa vyote vya Uchaguzi vinavyohitajika mapema.

Pia, Dk. Zakia amewasisitiza kuwa siku ya Uchaguzi mnaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha Kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi; na kufanya mawasiliano na Msimamizi wa Uchaguzi pale ambapo utahitajika ushauri kuhusiana na masuala ya Uchaguzi uliopo.

Kabla ya kufungua Mafunzo hayo, wasimamizi hao na wasimamizi wasaidizi hao walikula kiapo cha kutunza Siri na Kujitoa uachama wa Chama cha Siasa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Safia Iddi Muhammad.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza siku ya Jumamosi ya Juni 8, 2024 kuwa ni siku ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kwahani. Vyama 14 vya siasa vimejitokeza na vinaendelea na kampeni kuelekea siku ya uchaguzi.

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...