Majaliwa atoa wito kwa wanaotekeleza Afua za Wanawake

*Awataka watumie taarifa za na takwimu za sensa kuandaa mipango yao

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wadau wanaotekeleza afua mbalimbali za wanawake watumie taarifa na takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika kuandaa mipango na mikakati ya uwezeshaji wa wanawake nchini.

Mbali na hayo pia Majaliwa amewasisitiza wadau hao wanaotekeleza afua za wanawake waandae mipango yao kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali. “Hii ni namna bora ya kuharakisha ustawi na maendeleo ya wanawake.”

Majaliwa ameyasema hayo Jumamosi, Mei 18, 2024 katika hafla ya utoaji wa tuzo ya Malkia wa Nguvu iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Kwa Tunza Beach jijini Mwanza.

Pia, Waziri Mkuu amesema kuanzia Julai 2024 Serikali itatoa utaratibu wa namna ya uendeshaji na utoaji wa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

“Nitoe rai kwa wanawake wote na makundi ya vijana na watu wenye ulemavu wazingatie utaratibu utakaotolewa na niwakumbushe kuwa fedha inayotolewa ni mikopo siyo ufadhili hivyo wanufaika wote wawajibike kuirejesha,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutoa kipaumbele katika masuala ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa makundi maalum ya wanajamii likiwemo kundi la Wanawake.

Amesema Serikali kwa mwaka 2023/2024 imetenga kiasi cha Sh bilioni 18.5 kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo kwa riba ya asilimia saba na kufanya makubaliano na NMB yatakayowezesha wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wanawake kupata mikopo yenye riba nafuu.

“Ninafuraha sana kwa kuwa hamasa inayotokana na ushiriki wa Tuzo ya Malkia wa Nguvu imeendelea kuwavuta wanawake wengi zaidi na kuwafanya waongeze ubora wa shughuli wanazozifanya sambamba na kukuza biashara zao,” amesema.

Amesema anafahamu kuwa moja ya malengo ya Mradi wa Malkia wa Nguvu ni kuimarisha fursa za ajira na kuwa kichocheo muhimu cha uzalishaji wa ajira mpya.

“Ninawapongeza sana kwa kuchangia jitihada za Serikali katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana,” amesema.

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this