Burundi kuendelea kuwatuma wagonjwa wa moyo kutibiwa JKCI

Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam

Wataalamu wa afya kutoka nchini Burundi wametembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kuona namna ya kushirikiana katika matibabu ya moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Peter Kisenge alisema JKCI sasa inavutia nchi nyingi kutaka kujifunza kutokana na uwekezaji wa kisasa uliofanywa na Serikali.

Dk. Kisenge alisema nchini nyingi za Afrika zikitaka kuanzisha Hospitali za moyo zimekuwa zikifanya ziara katika taasisi hiyo kujifunza na kupata uzoefu ili nazo ziweze kufanikiwa.

“Wataalamu hawa kutoka Burundi wamekuja hapa kujionea nini tunafanya lakini pia kuweka mahusiano nasi ili waanze kuwaleta wagonjwa kutoka Burundi kuja kutibiwa JKCI. Tumekuwa tukitembelewa na wataalamu kutoka nchi tofauti kujifunza ikiwemo Somalia, Sierra Leon, Kenya na Burundi,” alisema Dk. Kisenge.

Dk. Kisenge alisema dhana ya tiba utalii katika taasisi hiyo imeongezeka kwa kasi kwani kwa kipindi cha miezi mitatu wameweza kuona wagonjwa kutoka nje ya nchi zaidi ya 365.

“Tumekuwa na wigo mkubwa wa kutoa huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo hivyo kupelekea kupata idadi kubwa ya wagonjwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika, lakini pia kutembelewa na wataalamu wa afya kutoka nje ya nchi ili waweze kujifunza hapa kwetu,” alisema Dk. Kisenge.

Dk. Kisenge alisema kupitia wagonjwa wanaotoka nje ya nchi uchumi wa nchi na wamtu mmoja mmoja unaongezeka kwani wanapokuwa hapa nchini wanajihusisha na shughuli tofauti zikiwemo za malazi, utalii na zinginezo.

Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Burundi Constantin Nyamuzangula alisema Tanzania imepiga hatua kubwa katika eneo la matibabu ya magonjwa ya moyo.

Dk. Constantin alisema kupitia ziara hiyo wamejifunza kuwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete inafanya upasuaji wa moyo wa aina karibuni zote, kwani nchini Burundi bado hawajaanza kufanya upasuaji wa moyo wa aina nyingi.

“Tumetembelea maeneo mbalimbali ya taasisi hii, wanaona wagonjwa wengi sana mazingira ya hospitali pia ni mazuri mtu akiwa hapa ni kama yupo eneo linalojihusisha na mambo mengine na si hospitali,” alisema Constantin.

Dkt. Constantin alisema kwa sasa Burundi inapeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa nchini Ufaransa, Beljium, Kenya na India lakini baada ya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wanaenda kuangalia namna ya kuwaleta wagonjwa kutoka Burundi kuja kutibiwa nchini kwani gharama za matibabu kwa Tanzania zipo chini tofauti na nchi nyingine.

Naye Mkuu wa Hospitali ya Shifaa iliyopo nchini, Burundi, Dk. Ndikumana Sudi alisema ujio wao katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete umewapa nafasi ya kujifunza mengi kutokana na huduma zinavyotolewa kupitia mifumo ya kisasa kwani kwao yapo mengi bado hawajafikia.

Dk. Ndikumana ambaye pia ni bingwa wa magonjwa ya sukari alisema wakati wa ziara yao wameweza kutembelea wodi za wagonjwa na kuongea na wagonjwa ambao wameonesha imani kubwa na taasisi hiyo kutokana na huduma wanazozipata.

“Sisi kwetu hatuna mtambo wa cathlab unaotoa huduma za upasuaji wa tundu dogo, lakini pia tumeona hapa wagonjwa wa ICU kila mgonjwa ana muuguzi wake hii inachangia katika kutoa matibabu bora,” alisema Dk. Ndikumana.

spot_img

Latest articles

Yanga kuikabili TRA bila Depu, kocha aeleza ugumu ulipo

Na Mwandishi Wetu WAKATI Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Machi 18, 2026  kuikabili TRA United katika Ligi...

Vijana 3,967 waomba uwezeshaji kupitia Go Green na IMBEJU ya CRDB Bank Foundation

Na Mwandishi wetu JUMLA ya vijana 3,967 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamewasilisha maombi ya...

RC Kunenge aipongeza Dawasa, awapa jukumu madiwani

Na Mwandishi wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema ushirikishwaji wananchi kwenye...

Serikali yatoa maelekezo nane kuimarisha kampuni ambazo ina umiliki hisa chache kuelekea Dira 2050

Na Mwandishi wetu, Arusha SERIKALI imetoa maelekezo nane ya kimkakati yanayolenga kuimarisha utendaji wa kampuni...

More like this

Yanga kuikabili TRA bila Depu, kocha aeleza ugumu ulipo

Na Mwandishi Wetu WAKATI Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Machi 18, 2026  kuikabili TRA United katika Ligi...

Vijana 3,967 waomba uwezeshaji kupitia Go Green na IMBEJU ya CRDB Bank Foundation

Na Mwandishi wetu JUMLA ya vijana 3,967 kutoka maeneo mbalimbali nchini wamewasilisha maombi ya...

RC Kunenge aipongeza Dawasa, awapa jukumu madiwani

Na Mwandishi wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema ushirikishwaji wananchi kwenye...