Askofu Bagonza: Mawazo ya Samia yametekwa

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan akisukuma mbele falsafa ya “R” nne yaani Maridhiano (Reconciliation), Mabadiliko (Reforms), Ustahimilivu (Resilience) na Kujenga Upya (Rebuild), kuna uwezekano kuwa mawazo yake yametekwa na watu wasiojulikana ambao wanapotosha juhudi hizo.

Akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Jukwaa la Demokrasia linalofanyika Zanzibar, Askofu Benson Bagonza bila kuwataja, alisema kuwa watu hao wanapotosha juhudi hizo ili kuukwamisha mkakati huo na hatimaye waje kumlaumu Rais Samia.

“Nina kila sababu kusema mawazo yake (Rais Samia) yametekwa na watu nisiowajua, wanaojaribu ama kuyapotosha au kuyatumia kuchelewesha ili mkwamo huu uendelee na baadaye waje kumlaumu Rais Samia,”
alisema Askofu Bagonza.

Bagonza alisema kuwa ukichunguza kwa makini R4 za Rais Samia ambazo alizifananisha na matofali ya kujenga upya taifa, ni kielelezo cha kukiri kwamba kuna kitu kilikwenda mrama katika maisha ya kisiasa ya taifa la Tanzania.

“Ujasiri huu wa Rais Samia, ni toba ya kiuungwana inayohitaji kufanyiwa kazi kwa umakini uliojaa uzalendo,” alisisita na kuonya kuwa si haki kuchukulia falsafa hiyo kama kauli mbiu ya kisiasa tu, kwani kufanya hivyo hakutalitendea haki taifa.

Alionya kuwa falsafa ya R4 imekwamishwa, huku akirejea kuhoji kuwa hadi sasa Tanzania tumeridhiana na nani, kwa sababu kadri siku zinavyosonga mipasuko inaongezeka kama inavyodhihiri sasa juu ya kuibuka kwa U-Tanganyika, Uzanzibari, Uzanzibara, Udini, Uchawa na Uchama.

Katika hutuba hiyo pia alihoji ni nini hasa kimebadilika, kwani badala ya kubadili sheria zinabadilishwa maneno na majina tu.

Pia alihoji ni nini kimejengwa kwani kuna mwelekeo wa watu kukusanya kuni ili kuchomana, hasa ikizingatiwa kwa sasa kwamba watu wanajenga Tanganyika isiyo na Tanzania na Zanzibar isiyo na Tanzania.

Bagonza alitoa angalizo kuwa uongozi wa Tanzania chini ya chama kinachoongoza, uwahakikishie wananchi kuwa lolote linaweza kufanyika, lakini si kurudi tena katika giza totoro lisilomhakikishia yeyote usalama.

Aliongeza: “Nionavyo mimi, ile “R” ya kwanza, yaani maridhiano inahitajika katika “R” nyingine zote zilizobaki (Mainstreamed).”

Bagonza alisema mfumo wa kidemokrasia nchini una walakini mwingi kama, kuruhusu mtu kupiga kura, lakini si kuchagua; kuwezesha wanaochaguliwa kuwa juu ya wanaochagua kuliko kinyume chake na kuruhusu mtu kutoa mawazo yake, lakini si kumhakikishia ulinzi ndani au nje ya chama chake.

Kadhalika, alisema mfumo wa demokrasia unaruhusu udikteta wa mtu au kundi moja uliofichwa ndani ya chama na unaruhusu wenye fedha kuwa na maamuzi juu ya wasio na fedha.

Mkutano wa Jukwaa hilo unahudhuriwa na watu mbalimbali kutoka vyama vya siasa, wasomi, vyama vya kiraia, huku pia wakiwamo washiriki kutoka Kenya na Afrika Kusini.

Mkutano huo wa siku mbili unaendeshwa chini ya kauli mbiu isemayo Kuelekea Demokrasia Jumuishi na Shirikishi.

Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Kituo cha Kesi za Kimkakati (Center for Strategic Litigation -CSL).

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...