Marubani wasinzia nusu saa ndege ikiwa angani

Mamlaka za nchini Indonesia zinachunguza tukio la marubani wawili wa ndege ya kampuni ya Batik Air ya nchini humo, waliogundulika kuwa walisinzia kwa dakika 28 wakati wa safari ya ndege yao.

Marubani hao wanaume ambao wamesimamishwa kazi kwa muda hivi sasa, walilala usingizi Januari 25, 2024 walipokuwa wakiendesha ndege kutoka mji wa Sulawesi kwenda mji mkuu wa nchi hiyo, Jakarta.

Ndege walioyokuwa wakiiendesha aina ya Airbus A320 ilipoteza mwelekeo kwa muda mfupi, lakini ilitua salama, na abiria wote 153 pamoja na wafanyakazi wanne hawakudhurika.

Vipimo vya kiafya walivyofanyiwa kabla ya safari vinaonyesha kwamba hawakuwa na tatizo lolote na hali zao ziliwaruhusu kurusha ndege.Mzunguko wa damu na mapigo ya moyo yalikuwa ya kawaida na hawakuwa wamekunywa kileo chochote.

Hata hivyo vipimo hivyo havikuweza kuthibitisha iwapo marubani hao walikuwa wamepumzika vya kutosha, alisema mtaalam wa anga za juu Alvin Lie.

Taarifa zinasema mmoja wa marubabi hao alikuwa amechoka kutokana na kukesha akisaidiana na mke wake kuwalea watoto wao pacha ambao ni wachanga.

Takriban nusu saa baada ya kupaa, Rubani Mkuu mwenye umri wa miaka 32 alimuomba rubani mwenzake kuchukua udhibiti wa ndege hiyo, akisema alihitaji kupumzika.

Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya uchukuzi, rubani msaidizi mwenye umri wa miaka 28 alikubali lakini muda mfupi baadaye, naye alipitiwa na usingizi.

Kulingana na ripoti hiyo, mkewe alikuwa ametoka tu kujifungua watoto pacha wa mwezi mmoja na alikuwa akisaidia katika malezi ya watoto wao.

Waongoza ndege kwenye Uwanja wa ndege wa Jakarta walijaribu kuwasiliana na chumba cha marubani cha Batik Air A320, lakini hawakujibiwa.

Kimya hicho kilidumu kwa dakika 28 hadi rubani kiongozi alipoamka na kugundua kuwa rubani mwenzake naye alikuwa amepitiwa na usingizi.

Pia aligundua kuwa ndege hiyo ilikuwa imeacha njia kwa dakika kadhaa.

Baada ya kuamka, Rubani Mkuu aliitika wito kutoka Jakarta, hivyo kupata maelekezo ya mwongozo uliowezesha ndege hiyo kutua salama.

Mamlaka sasa “imeonya vikali” Batik Air kuhusu tukio hilo, na M Kristi Endah Murni, kiongozi wa usafirishaji wa anga za juu wa Indonesia, anasema Shirika hilo la ndege linapaswa kutilia maanani muda wa kupumzika kwa wafanyakazi wake.

Batik Air kwa upande wake linasema “sera yake inazingatia muda wa kutosha wa mapumziko kwa wafanyakazi wake na kuahidi kutekeleza mapendekezo yote ya kiusalama”.

Mnamo mwaka wa 2019, ndege hiyo hiyo ililazimika kutua dharura baada ya rubani kupoteza fahamu.”

spot_img

Latest articles

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi yaanza kazi, yakaribisha wananchi kutoa maoni

Na Winfrida Mtoi Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi nchini, imesema tayari imeanza...

Urathi wa Mwalimu Nyerere usaidie kukubali kukosolewa

JUMATATU wiki hii Watanzania walikumbuka kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki...

Nimemsikiliza Gachagua, nikatamani Lowassa 2008 angelipambana vivyo

KWA zaidi ya wiki mbili sasa majirani zetu, Kenya, kumekuwa na siasa za moto....

Kukataa mgombea binafsi ni kukumbatia utumwa

HISTORIA inashuhudia kwamba wapo watumwa walikataa kuwa huru kwa sababu waliamini kwamba pamoja na...

More like this

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi yaanza kazi, yakaribisha wananchi kutoa maoni

Na Winfrida Mtoi Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi nchini, imesema tayari imeanza...

Urathi wa Mwalimu Nyerere usaidie kukubali kukosolewa

JUMATATU wiki hii Watanzania walikumbuka kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki...

Nimemsikiliza Gachagua, nikatamani Lowassa 2008 angelipambana vivyo

KWA zaidi ya wiki mbili sasa majirani zetu, Kenya, kumekuwa na siasa za moto....