Yanga kuikabili TRA bila Depu, kocha aeleza ugumu ulipo

Na Mwandishi Wetu

WAKATI Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani kesho Machi 18, 2026  kuikabili TRA United katika Ligi Kuu Tanzania, timu hiyo itawakosa wachezaji wake muhimu wanaokabiliwa na majeraha akiwamo mshambuliaji Laurindo Dilson ‘Depu’.

 Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea  mchezo huo utakaopigwa kesho saa 10:00 alasiri, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves  amesema wamekuwa na ratiba ngumu ya michezo mfululizo ukizingatia wametoka kucheza mechi ngumu siku chache zilizopita tofauti na wapinzani wao.

Amesema wanakwenda kukabiliana na timu ambayo imepata muda wa kutosha wa mapumziko na maandalizi lakini wamejipanga kuchukua pointi tatu.

“Pia tumekubwa na idadi kubwa ya majeruhi. Lakini hali hiyo inatoa fursa kwa wachezaji wengine wenye hali nzuri,” amesema.

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa taarifa ya  kuthibitisha kuwa wachezaji wake wanne wakiwemo  Chadrack Boka, Edmund John pamoja na Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ wamepata majeraha na wanatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa.

Wachezaji wengine ni Chadrack Boka ambaye amepata jeraha la enka ya mguu wa kushoto na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili, na Edmund John ambaye amepata jeraha la bega na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.

spot_img

Latest articles

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...

TIRDO yasajili Viwanda 25,650, Yaongeza Maabara za Kisasa Kuimarisha Sekta ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya...

MD Twange aeleza kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa mradi wa Hale

📍Ni ule wa kuboresha kituo cha kufua umeme 📍Amuagiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa...

More like this