Madarasa, funza vyatishia usalama wanafunzi Mwanga

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlevo iliyopo katika Kijiji cha Kilomeni, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, wapo hatarini kutokana na uchakavu wa madarasa wanayotumia, kujaa kwa vyoo na kushambuliwa na funza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, wamesema tangu shule hiyo ijengwe mwaka 1975 haijawahi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote.

Mmoja wa wazazi, Stela Mcharo amesema mazingira ya wanafunzi kujisomea shuleni hapo si mazuri na baadhi miguu yao huliwa na funza wanaokaa kwenye vumbi la madarasani.

“Mimi ni mzazi ninayesomesha watoto hapa, nasikitika sana kwa hii shule yetu, haina madirisha wala milango, majengo ya shule ni chakavu, watoto wanaliwa funza,” amesema mzazi huyo.

Mcharo amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan asikie kilio chao.

“Watoto wetu wanapata taabu sana, hawana pa kusomea hata hawa walimu ambao wapo hapa wanafundisha pia funza wanawaingia miguuni.”Alipotafutwa kwa simu,

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Zahara Msangi aliomba apewe muda kwenda kuangalia hali ilivyo katika shule hiyo na kwamba leo mchana na timu yake imeelekea kuangalia hali ilivyo katika shule hiyo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilomeni, Joseph Msangi amekiri kuwepo kwa uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo na kwamba mara kadhaa wamekuwa wakitafuta wafadhili kuibuka changamoto za hapa na pale.

“Nimepambana na uongozi wa halmashauri ya kijiji na diwani wa kata hii angalau tupate fedha au wafadhali wa kutusaidia kujenga hii shule kwa sabau siku zote imekuwa ni chakavu, lakini bado kuna changamoto zinazojitokeza,” amesema.

Akizungumzia changamoto ya miundombinu ya shule hiyo, Diwani wa Kata ya Kilomeni Mohammed Mgala, amesema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo lakini hakuna kinachotekelezeka.

“Shule hii ilianza mwaka 1975 wakati wa UPE (elimu ya msingi kwa wote) ili kuwezesha wanafunzi kwenda shule, kwa hiyo ilijengwa kwa taratibu ambazo si za viwango na ndio imetufikisha hapa tulipo.

“Tunashukuru Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kujenga shule hii lakini haijengwi, mwaka jana shule hii ilipewa Sh50 milioni, mwaka huu imepewa Sh67 milioni kwa ajili maboresho mbalimbali lakini haijengeki,” amesema Mgala ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo.

“Shule imepewa fedha za vyoo zaidi ya Sh10 milioni lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika,” ameongeza Mgala, bila kufafanua fedha hizo zimekwenda wapi,” alisema.

CHANZO: MWANANCHI

spot_img

Latest articles

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...

Rais Samia kuzindua Dira ya Taifa ya 2050

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa...

More like this

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...