Mzee Mwinyi kuzikwa Mangapwani Unguja

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, atazikwa kesho Jumamosi Machi 02, 2024 saa 10:00 alasiri Kijijini kwakw cha Mangapwani, Unguja visiwani Zanzibar.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, shughuliza mazishi ya kitaifa zinaanza leo ambapo mwili wa Mzee Mwinyi utaagwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ataongoza waombolezaji katika mazishi ya kitaifa yatakayofanyika kesho asubuhi, Uwanja wa Amaan Zanzibar, kabla ya kwenda kuzika kijijini Mangapwani.Kwa mujibu wa ratiba hiyo, leo Ijumaa Machi 1, 2024 saa 5:30 asubuhi; mwili wa Hayati Mzee Mwinyi utaondoka nyumbani kwake Mikocheni, Dar es Salaam kuelekea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni, ambako Sheikh Mkuu wa Tanzani, Dk. Abubakar Bin Zuber Bin Ali ataongoza swala ya Ijumaa pamoja na taratibu zote za kidini.

Majaliwa amesema saa 8:00 mchana; mwili wa kiongozi huyo utaondoka kuelekea Uwanja wa Uhuru ambako milango ya uwanja itakuwa wazi kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya wananchi na viongozi mbalimbali kushiriki maombolezo.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kuanzia saa 8:30 mchana, Dua na maombi kutoka kwa viongozi wa dini na salamu za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali zitatolewa, na kufuatiwa na utoaji wa heshima za mwisho.

Amesema Saa 11:00 jioni; mwili wa Hayati Mzee Mwinyi utaondolewa uwanja wa Uhuru kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kisha kusafirishwa kwenda Zanzibar.

Inatarajiwa kwamba saa 11:30 jioni; Wananchi wa Zanzibar na maeneo mengine ya Unguja watapokea mwili huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume na kuelekea nyumbani kwa marehemu.

*MAZISHI YA KITAIFA ZANZIBAR* Waziri Mkuu Majaliwa amesema, kesho Jumamosi Machi 02, 2024, milango ya uwanja wa Amani itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambako mazishi ya kitaifa yatafanyika.Viongozi wanatarajiwa kuanzia kuigia uwanjani hapo saa 3:00 asubuhi ili kuupokea mwili wa Hayati Mzee Mwinyi unaotarajiwa kuwasili kuanzia saa 04:00 asubuhi kwa ajili ya maombolezo ya kitaifa na kutoa heshima za mwisho.

Amesema saa 5:00 asubuhi viongozi wa dini wataogoza Dua na swala, zikifuatiwa salaam za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali kuanzia saa 5.30 asubuhi. Tukio hilo litahitimishwa na salaam za pole za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Saa 6:30 mchanaviongozi na wananchi watatoa heshima za mwisho na saa 9:00 alasiri mwili wa Hayati Mzee Mwinyi utaondoka uwanja wa Aman kuelekea kijijini kwa marehemu Mangapwani kwa ajili ya mazishi ya Kitaifa yatakayofanyika Saa 10:00 alasiri.Majaliwa amesema itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu matukio ya kila hatua kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali.

Mzee Mwinyi alifariki dunia jana Februari 29, 2024 saa 11.30 jioni katika Hospitali ya Mzena alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu ya saratani ya mapafu.

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...