Msafara wa Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda umepata ajali katika eneo la Masasi mkoani Mtwara.
Ajali hiyo iliyotokea saa 9 alasiri imehusisha zaidi ya magari 7 yaliyokuwa kwenye msafara huo, uliokuwa unatokea mkoani Ruvuma kuelekea, Dar es Salaam.
Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa takriban watu 7 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospital ya Mkoa wa Mtwara [Ligula] kwa ajili ya matibabu. Hakuna kifo kilichoripotiwa.
Chanzo: Mwanahabari Digital